loader
Ndayiragije matumaini kibao

Ndayiragije matumaini kibao

KOCHA wa muda wa timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema anaimani kikosi hicho kitapata ushindi kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Kenya. Stars na Harambee zinatarajiwa kurejeana mwishoni mwa wiki hii mjini Nairobi katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani Chan, baada ya kutoka suluhu kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam juzi.

Akizungumza baada ya mechi ya juzi, Ndayiragije alisema kulingana na mchezo waliouonesha wachezaji wake juzi bado wanaonekana wananguvu ya kupambana kusaka ushindi kwenye mechi ya mwisho itakayoamua hatima ya nani atasonga mbele.

“Wachezaji wamecheza vizuri,isipokuwa walikosa mambo kadhaa ya kiufundi ninapaswa kama kocha kuyafanyia maboresho katika kipindi hiki kifupi,ninaimani wanauwezo wa kupambana na tutapata matokeo licha ya mchezo wetu wa marudiano utakuwa na presha kwa sababu tutakuwa ugenini,” alisema.

Kwa upande wake nahodha wa kikosi hicho John Bocco aliwataka mashabiki kutorudi nyuma na kukata tamaa ya kuendelea kuwasapoti kwa kuwa hayo ni matokeo ya mpira huku akiahidi kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudiano. “Mashabiki walikuwa na matarajio makubwa ya kuvuna ushindi lakini mambo yamekuwa tofauti kiufupi benchi la ufundi limeona mapungufu na watayafanyia kazi ili kwenye mchezo wa marudiano tukapate matokeo,”alisema Bocco.

Katika mchezo huo ambao stars walitawala kwa vipindi vyote walionekana kukosa ubunifu sehemu ya umaliziaji na hivyo kukosa mabao mengi. Kwa upande wake kocha wa kikosi cha Harambee Stars Sebastien Migne aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonesha mchezo mzuri wa ugenini hasa kipindi cha pili lakini kukosa utulivu sehemu ya kumalizia kuliwakosesha ushindi.

“Timu yangu imecheza vizuri hasa kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko lakini tulishindwa kutumia nafasi za mwisho bado tunakibarua kigumu kwenye mchezo wa pili ambao bado nauona mgumu kwetu sote kwa sasa viwango bado tunafanana sijaona utofauti mkubwa,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ab4fbfcc8a53bf89cfff9af21e54d792.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Na Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi