loader
Makonda kusaidia wanawake walioachwa

Makonda kusaidia wanawake walioachwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema, hafurahii kuendelea kuongoza wanawake walioumizwa mioyo kwa kuahidiwa kuolewa na kuachwa.

Amesema, ataangalia namna ya kukomesha tabia ya wanaume waliooa kuwa na mahusiano nje ya ndoa zao na kuwadanganya wanawake kuwa watawaoa.

Ametoa mwito kwa wanaume wanaopenda kuahidi ndoa watoe mawazo yao kuhusu jambo hilo na kwamba, huenda baadhi yao wanahitaji maombi tu.

“Inawezekana ukaona ni jambo la kawaida kwa sababu hujawahi kuumizwa katika mahusiano lakini walioumizwa wanajua mateso waliyokuwanayo na ndio maana hata akija kazini ana hasira tu kumbe kuna mtu ameshamuumiza, inapunguza hata performance ya utendaji wake wa kazi”amesema Makonda ofisini kwake.

Amesema, ipo haja ya kuwaita akina dada walioahidiwa kuolewa na wakaachwa ili wasaidiwe na hatimaye Dar es Salaam iwe yenye amani na utulivu kwa kuwa usalama wa taasisi ya ndoa ni usalama wa jamii na taifa kwa ujumla.

“Lakini yapo mawazo ya kwamba yawezekana tuanzishe database (kanzi data) ya kuingiza taarifa za ndoa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo itamwezesha binti akiahidiwa kuolewa ana uwezo wa kuingia kwenye hiyo data base akaangalia jina…”

Amesema itaanzishwa kanzi data yenye taarifa sahihi za ndoa za kiislamu na kikristu na kwamba, vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) vitasaidia kufanikisha hilo.

“kama ni mwanaume anaitwa Paul Makonda ataingia ataangalia, kama ni ahadi ya ndoa atapata taarifa huyu ameoa, na kama ameoa atajua cha kufanya, lengo ni kuwaepusha akina dada wasiendelee kuumia na matapeli wanaoahidi kuwaoa na mwisho wa siku wanatumia mali zao, na kuwatumia, na kuwa-abandon (kuwaacha) bila kuendeleza kutumia ndoto walizokuwanazo”amesema.

Amesema, anatumaini kutakuwa na mjadala mpana kwa kuwashirikisha wananchi na kwamba, Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali utatumika kupata mawazo na uzoefu wa nchi nyingine kuhusu jambo hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7709e6ebfcbad576e31fd786224df83b.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi