loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JK atoa msisitizo viwanda SADC

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema kufanana kwa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) isemayo ‘Mazingira Wezeshi ya Biashara kwa Ajili ya Maendeleo Jumuishi na Endelevu ya Viwanda’ na kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano isemayo Tanzania ya Viwanda, ni uthibitisho kuwa sekta ya viwanda ndio tegemeo muhimu katika kuzikomboa kiuchumi nchi za Kusini mwa Afrika.

Aidha Rais huyo Mstaafu ametaja mambo manne makubwa ambayo ni mafanikio ya kujivunia kwa SADC tangu ilipoundwa mwaka 1980 na kutaja kasoro ambazo ni lazima zifanyiwe kazi haraka na viongozi wa nchi wanachama ili kuweza kufikia malengo.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipofanya mahojiano maalumu na vyombo vya habari vya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL).

Akizungumzia kufanana kwa kaulimbiu hizo katika kuhamasisha maendeleo endelevu ya viwanda; Kikwete alisema kaulimbiu hizo ni nzuri kwani zinahamasisha mambo ya msingi katika kuyawezesha mataifa ya Kusini mwa Afrika kujenga mazingira wezeshi katika maendeleo ya viwanda na hasa kwa kutumia sekta binafsi.

Alisema pamoja kuwepo kwa wazo la kuzifanya nchi za SADC kuingia katika mtangamano wa kiuchumi, lakini bado nchi nyingi za jumuiya hiyo hazifanyi vizuri ukiachilia mbali Tanzania aliyosema inatekeleza kwa kasi Sera ya Maendeleo ya Viwanda ambayo sasa inaashiria kuiwezesha nchi kuingia katika uchumi wa kati ndani ya muda wa mwaka mmoja hadi miwili ijayo.

“Sisi lengo letu kama nchi tangu tulipoanza kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Viwanda ya Miaka Mitano ilikuwa ni kuiwezesha nchi kuingia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 lakini pia kukuza pato la mwananchi kutoka Dola za Marekani 3,000 kwa mwaka,” alisema Kikwete.

Alisema hata hivyo mataifa hayo ya SADC yanakabiliwa na changamoto ya kuweza kuboresha mu la kupigania ukombozi Kusini mwa Afrika na sasa kujikita katika maendeleo ya kiuchumi, kuondoa mfumo wa zamani wa nchi kuratibu shughuli za kisekta na sasa kuundwa kwa Sekretarieti, kuanzishwa kwa chombo maalumu cha kushughulikia masuala ya siasa, ulinzi na usalama ndani ya jumuiya, na kuanzishwa kwa programu kubwa za uchumi na siasa.

“Hatua ya kubadilika kimuundo kwa Sadc ya zamani yenye C mbili kuwa yenye C moja baada ya Afrika Kusini kuwa huru na Mandela (Nelson) kuwa Rais na kuifanya sasa jumuiya kujikita zaidi kwenye shughuli za kiuchumi na si ukombozi bila kutokea kwa migogoro, haya naweza kuyaita kuwa ni mafanikio makubwa. “Lakini pili ni kuondoka katika mfumo wa zamani wa nchi kuratibu shughuli za kisekta na kuundwa kwa Sekretarieti ambayo sasa ndiyo inasimamia shughuli za hizo za kisekta kwa mafanikio makubwa ni jambo la kujivunia. “Lakini pia kuanzishwa kwa organi ya utatu iitwayo Troika ambayo inasimamia masuala ya siasa, ulinzi na usalama ndani ya jumuiya kumeleta mafanikio makubwa sana. Hivi sasa wanafanya kazi kubwa sana, SADC sasa si jumuiya ya migogoro sana ni kama nchi mbili tu ambazo zimekuwa na migogoro ya kisiasa,” alisema Kikwete.

Akizungumzia mtangamano wa kiuchumi, Kikwete alisema bado viongozi wa jumuiya hiyo hawajafanya vizuri sana katika kufuma uchumi wa nchi hizo kuwa uchumi mmoja na kutoa rai kuwa ni lazima kazi hiyo ifanyike haraka na eneo la kuanzia ni katika sekta ya biashara. mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuweza kuwiana na vigezo vilivyowekwa na Benki ya Dunia, Jukwa la Dunia la Kiuchumi (WEF) na Taasisi ya Mo Ibrahim ili kuweza kuvutia sekta binafsi kusaidia kukuza uchumi wa mataifa hayo.

“Ni jambo muhimu sana kuhamasisha mazingira ya uwekezaji, na ni vizuri viongozi wameliona umuhimu wa kuzungumzia suala hili na wasiishie katika kujadili tu, wachukue hatua madhubuti, wakifanya hivyo, uwekezaji utakua, viwanda vitakua na hasa kwetu sisi ambao tunaazimia kuwa na Tanzania ya Viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema Kikwete.

Ataja mafanikio ya SADC Akizungumzia mafanikio anayoyaona tangu kuundwa kwa SADC, Rais Mstaafu Kikwete alitaja maeneo manne ya mabadiliko ya kimuundo kutoka Sadc ya mwanzo iliyokuwa na juku- “SADC wana kazi kubwa ya kufanya katika eneo hili, wanaweza kuangalia mfumo unaotumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Huku kwenye EAC kazi iliyofanywa katika kutengeneza mtangamano wa kiuchumi ni kubwa na nzuri, walianza na Itifaki ya Soko la Pamoja ili kuweza kufuma uchumi wa pamoja kwa kuondoa vikwazo vya kikodi na kulinda bidhaa za ndani ya jumuiya dhidi ya zile zinazotoka nje, kwa SADC hili bado halijafanyika.

“Kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wao waliondoa kodi kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi wanachama, lakini kwa SADC naona nchi zimepewa uhuru wa kuamua zenyewe, ni vizuri viongozi wakatumia mkutano huu kujadili na kuchukua hatua,” alisema.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi