loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Coutinho atua Bayern kwa mkopo

MCHEZAJI wa Barcelona, Philippe Coutinho, ametua Ujerumani kwa ajili ya kuichezea Bayern Munich kwa mkopo wa muda mrefu katika msimu huu. Mbrazili huyo alikuwa akipambana ili kufiti katika kikosi cha Barcelona tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Liverpool Januari 2018.

Coutinho, 27, hivi karibuni alikubali maslahi binafsi na mabingwa hao wa Ujerumani, ambao wanakamilisha baadhi ya mambo ya kiutawala na Barca. Mchezeshaji huyo wa zamani wa Liverpool anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Bayern Munich baada ya Barca kupitia mkurugenzi wao wa mahusiano, Guillermo Amor kusema kuwa anathibitisha kuwapo makubaliano ya kumchukua kwa mkopo Coutinho.

“Naweza kuthibitisha kuwa kuna makubaliano ya kimsingi kuhusu Coutinho kuichezea kwa mkopo Bayern,”alisema Amor.

Coutinho aliachwa katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga kati ya Barca na Athletic Bilbao, lakini alionekana katika picha akiwa jukwaani siku hiyo ya mchezo huo. Walipoulizwa jana kuhusu uhamisho wa mkopo wa mchezaji huyo, klabu hiyo ya Catalan ilisema hawana mpango naye isipokuwa hadi pale watakapomnasa Neymar.

Coutinho katika kipindi chote cha majira ya joto amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Nou Camp. Lakini kuondoka kwa mshambuliaji huyo kunaweza kumaliza ndoto ya Neymar kutaka kurejea Barca. Paris Saint-Germain iliweka wazi kuwa inataka kumjumuisha Coutinho katika mpango wowote wa Neymar.

Real Madrid nayo pia imeonesha nia ya kutaka kumsajili Neymar katika kipindi hiki cha majira ya joto, lakini hivi karibuni iliripotiwa kuwa ilishindwa kutoa fedha pamoja na mchezaji huyo baada ya PSG kung’ang’ania kiasi cha Pauni milioni 206.

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: MUNICH, Ujerumani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi