loader
Dstv Habarileo  Mobile
WCB yabariki kuondoka kwa msanii Harmonize

WCB yabariki kuondoka kwa msanii Harmonize

MMOJA wa mameneja wa Lebo ya WCB Wasafi, Sallam Sharaf amethibitisha kuwa msanii Harmonize ‘Konde boy’ yuko mbioni kuachana na lebo (kundi) hiyo iliyomkuza kimuziki.

Salaam ameyasema hayo hivi punde wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano na moja ya vituo vya radio jijini Dar es Salaam, alisema “Harmonize ametuma maombi ya kuvunja mkataba na WCB wasafi , sisi hatuna shida ana baraka zetu zote…

“…hivi Karibuni amefanya sapraisi nyingi sana bila uongozi wa WCB kujua, lakini sisi tunataka misingi ya ofisini yetu iheshimiwe na lazima isimamiwe,”alisema Meneja huyo  mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Meneja huyo alienda mbali akisema kuwa Harmonize ndani ya Moyo wake hayupo WCB, lakini Kimkataba bado yupo WCB.

"Unapokubali kuingia kwenye mkataba ni sawa umeingia kwenye ndoa, Wasafi ni Taasisi huwezi kuingia tu na kutoka,” amesema Meneja huyo.

WASANII WA KUNDI HILO

WCB inaundwa na nyota wengine ambao ni Diamond Platnumz, Rayvanny, Queen Darleen, Lava Lava na Malomboso

MENEJA WA HARMONIZE

Kwa mujibu wa taarifa rasmi za WCB, Wasanii wote wa kundi hilo wana mameneja wakuu watatu, Said Fella ‘Mkubwa Fella’, Sallam Sharaff ‘SK’ na Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’ lakini kuna mameneja wanaomsimamia msanii mmoja-mmoja.

Kwa upande wa Harmonize, tangu mwaka 2018 alikuwa chini ya Meneja Joel  Joseph ‘Mr Puaz’ambaye naye alisainiwa WCB kumsimamia mwanamuziki Harmonize katika kazi zake. Moja kati ya mafanikio ya kazi kubwa alizofanya Meneja huyo ni kumjenga Harmonize na kuikuza sanaa yake ya muziki.

Katika kazi zilizoleta mafanikio makubwa kwa Harmonize chini ya meneja huyio ilikuwa ni "kwangwaru" ambayo ni kazi ilibadilisha maisha ya Harmonize na kumpa nafasi kubwa sana meneja huyo kuwa mmoja wa mameneja hodari wa Talanta Tanzania.

 

NGOMA ALIZOTOA HARMONIZR AKIWA WCB

Baadhi ya nyimbo alizotoa msanii huyo ni; Aiyola, Bado, Matatizo, Inde, Niambie, Show Me, Happy Birthday, Unaionaje, Sina, Shulala, Nishachoka, Pilipili, Kwa Ngwaru, DM Chick, Nimwage Radhi, Love You na Fire Waist.

KUWA MSANII WA PILI KUIKACHA WCB

Mbali na Harmonize ambaye amedhibitishwa kuwa yupo njiani kuachana na WCB, Msanii Rich Mavoko alikuwa wa kwanza kuachana na lebo hiyo mwanzoni mwa mwaka jana.

 

ALI KIBA AUSISHWA

Japo haijadhibitika lakini inaelezwa kuwa msanii huyo amekuwa na mawasiliano na Msanii Ali Kiba na lebo yake.

 

RAY VANNY AZUNGUMZA

Kwenye moja ya shoo juzi, Msanii wa kundi la WCB Rayvanny alifunguka kuhusu  Harmonize kudaiwa kuondoka WCB na kusema, “Mashabiki wanamtukana Harmonize mitandaoni, anaweza kuhisi wanatumwa na uongozi wa WCB kumbe sio.”

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi