loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkutano mwingine kuleta wajumbe 400

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema kufanyika kwa Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) ambao utakuwa na washiriki takribani 400, utatoa fursa lukuki kwa Tanzania.

Pia Bunge la Tanzania linakwenda kwenye mkutano huo kushawishi wanachama wa jumuia hiyo kuwekeza jijini Dodoma.

Spika Ndugai aliyasema hayo jijiji hapa wakati walipozungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mkutano huo utafanyika Zanzibar kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 5, mwaka huu na utafunguliwa Septemba 2, na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Alisema mkutano huo utajumuisha maspika, naibu maspika, wabunge na mabalozi kutoka nchi wanachama, maspika wa mabara mengine au kanda na kumekuwa na mwitikio mkubwa sana.

“Mpaka sasa Maspika 20 kutoka nchi wanachama wameshathibitisha ushiriki wao ikiwa ni pamoja na wabunge kutoka nchi hizo na wafanyakazi, wameonesha nia kubwa ya kushiriki hasa ikizingatiwa unafanyika kwenye mji wa kitalii,” amesema Ndugai.

Alisema mkutano unafanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu, lakini Bunge la Tanzania litatumia fursa hiyo kushawishi wanachama wa CPA kuridhiwa kwa sehemu kuwekeza katika ujenzi wa hoteli ya nyota tano jijini Dodoma ambayo tayari kiwanja kimepatikana.

“Tanzania ndio makao makuu ya CPA Kanda ya Afrika, kwa kuwa tuna kamfuko ketu ambacho nchi wanachama huchangia na sisi Tanzania ndio tunatunza kwa fedha za kigeni, hivyo tutashawishi wenzetu wakubali sehemu fulani ya fedha hizo kuwekeza Dodoma,” amesema Ndugai.

Alifafanua uwekezaji huo ni wakujenga hoteli hiyo ambayo itakuwa ni mali ya CPA na kiwanja kipo kikubwa jirani ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) na michakato mbali mbali ya awali imeshafanyika.

“Tutashawishi ili fedha hizo zibaki nchini kwetu kwa kuwekeza ili kujenga jiji la Dodoma, tutajenga hoteli ya kisasa kabisa, kwani tumekuwa tumekuwa tunapata shida tunapopata wageni wakubwa,” alisema.

Aidha, Ndugai alisema pia itakuwa ni fursa ya kuitangaza nchi katika sekta ya utalii na pia watoa huduma mbalimbali Zanzibar watanufaika na mkutano huo.

“Naomba kuwashauri wafanyabiashara na Watanzania kutumia fursa hizi tunazopata za kuaminiwa na mataifa mbali mbali, ni adhimu mataifa mengine wanazililia na hii tumshukuru Rais John Magufuli ambaye ameendelea kuipatia heshima nchi yetu,” alisema.

Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa CPA, Stephen Kagaigai alisema lengo ni kuufanya mkutano huo kufanyika kwa viwango kama Mkutano wa Jumuiya ya Mendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

“Makao makuu ya chama yapo Tanzania hapa bungeni, tumefanya maandalizi ya kutosha hadi sasa kuwapokea wageni na tunatarajia wageni kati ya 400-500 wataingia kuanzia Agosti 28, mwaka huu,” alisema Kagaigai.

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi