loader
Picha

Waziri Ndugulile kushiriki ‘Twende Pamoja’ Kigamboni

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile leo atazungumza na wakazi wa Kigamboni na maeneo jirani namna ya kulinda haki za wanawake na watoto.

Ndugulile, ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni, atazungumza na wakazi hao kwenye kongamano la Twende Pamoja, litakalofanyika katika Viwanja vya Mjimwema Kigamboni chini ya uratibu wa Shirika la Kupinga Manyanyaso dhidi ya Wanawake na Watoto(Sawa).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia katika wizara hiyo, Julius Mbilinyi alibainisha kuwa katika kongamano hilo yatajadiliwa masuala mbalimbali kuhusiana na haki za wanawake na namna ya kuwanasua dhidi ya ukatili huo.

Alisema wanawake na watoto nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa ambazo zinawakosesha uhuru, kuwanyanyasa, kuwadhurumu haki za huku wengine wakiteswa na kunyanyasika.

Mbilinyi alisema ili kukabiliana na changamoto kama hizo kwenye maisha kuna kila sababu ya jamii kushirikiana pamoja kwa kujadiliana njia mbadala zitakazowasaidia kuyakabili mateso hayo.

Alisema kwa kuanzia kwa Dar es Salaam litafanyika kongamano hilo ambalo alibainisha kuwa litaenda nchi nzima na kuwataka wadau wengine kadhaa kujitokeza kwa wingi kusaidia mapambano yanayowakosesha uhuru wanawake.

“Kesho (leo) jamii inakutana kwa pamoja kujadiliana mbinu za kuwasaidia wanawake na watoto kupata haki zao na kuwasaidia dhidi ya mateso wanayopata katika jamii, hizi ni harakati za Sheta ambazo zinapaswa kuungwa mkono na jamii nzima,” alisema.

Mwenyekiti wa Sawa, shirika linaloratibu Kongamano hilo, Nurdin Bilal maarufu kama Sheta alisema kuwa mkakati wa kongamano hilo ni kuwakutanisha pamoja wanajamii na wadau wengine wa haki za jinsia ili kushauriana na jamii mikakati ya kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji wa wanawake na watoto.

Alibainisha pia kuwa hakutakuwa na kiingilio huku akiwataka vijana wengi zaidi kujitokeza na kunufaika na elimu hiyo huku pia wakipatiwa burudani kutokea kwa wasanii kadhaa kama vile wa muziki wa kizazi kipya, vichekesho na wengineo kadhaa.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi