loader
Picha

Aweso aiasa Auwsa mradi wa maji

NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA) kuhakikisha ifi kapo Desemba mwaka huu maji safi ya visima 56 vilivyochimbwa na mradi mkubwa wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 520 yanaanza kuwafi kia wananchi ili waondokane na kero ya upungufu wa maji.

Akitoa agizo hilo jana jijini hapa wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya mradi huo, Aweso alisema mbali na visima hivyo, yamejengwa matanki 10 ya kuhifadhia maji ambayo kwa siku kupitia visima hivyo yatazalisha zaidi ya lita milioni 200 kwa saa, huku mahitaji yakiwa ni lita milioni 90 kwa saa.

“Maji yatakuwa mengi zaidi ya matumizi na hii itaondoa tatizo la maji na kulifanya historia. Ninachoomba wananchi wavumilie miezi michache hii wakati miundombinu inaendelea kukamilishwa ili waanze kuunganishiwa maji safi,” alisema.

Alisema ni vyema ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji la lita 10, 000, 000 linalojengwa kwenye eneo la Ngaramtoni ukakamilika mapema ili maji hayo yaanze kupelekwa kwa wananchi.

Akitoa mfano alisema kisima kilichopo eneo la Maji Moto wilayani Hai kitatoa maji lita 200,000 hadi 500,000 kwa saa, jambo litakalowezesha wananchi wa pembezoni mwa mabomba hayo yatakapopita kupata maji hayo. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Arusha (AUWSA), Ruthi Koya alisema tatizo la upungufu wa maji linakwenda kuisha baada ya Serikali kuwapa zaidi ya Sh bilioni 520.

“Upatikanaji maji utakuwa rahisi ifikapo Desemba mwaka huu. Naomba wananchi tuvumilie miezi hii michache tunapokamilisha ujenzi wa miundombinu,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa AUWSA, Dk Richard Masika alisema kukamilika kwa mradi huo kutawezesha Arusha kupata maji lita milioni 200 kwa siku, maji ambayo ni zaidi ya mahitaji yanayohitajika kwa siku.

Alisema wao kama bodi kazi yao kubwa ni kusimamia ipasavyo mradi huo ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kama ilivyokusudiwa. Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro alisema kukamilika kwa mradi huo kutawezewesha Arusha kuondokana na upungufu wa maji uliopo kutoka asilimia 44 hadi kupatikana kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2020, mradi huo utakapokamilika.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi