loader
Picha

NIDA: Kamilisheni vielelezo mpate vitambulisho

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoani Morogoro imewataka wananchi mkoani humo kukamilisha vielelezo muhimu vya maombi ya kupata vitambulisho hivyo ili waweze kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Usajili huo unafanywa chini ya mfumo mpya uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Ofisa Msajili wa mamlaka hiyo mkoani hapa, James Malimo alisema hayo juzi mjini hapa alipoelezea maendeleo ya kazi ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kwa Mkuu wa Mkoa, Dk Kebwe Stephen Kebwe.

Dk Kebwe alifanya ziara kwenye ofisi za mamlaka hiyo katika eneo la Tungi kwenye Manispaa ya Morogoro kwa lengo la kujionea kazi ya usajili kwa wananchi. Alisema kazi hiyo inaendelea vizuri kwa kushirikiana na kampuni za simu pamoja na TCRA. Aliongeza kuwa inachukua wiki mbili mtu kupata kitambulisho cha taifa, hasa kwa yule aliyekamilisha vielelezo vyake kama cheti cha kuzaliwa au cha shule.

“Tumesogeza huduma katika ngazi ya kata, tunapeleka namba hizo na mwananchi anaweza kwenda kusajili simu yake,” alisema Malimo.

Hata hivyo, alisema lengo la mkoa wa Morogoro ni kusajili wananchi 300,000 na hadi sasa usajili huo umefikia asilimia 75. Dk Kebwe aliwataka wananchi mkoani humu wahakikishe wanakamilisha kusajili namba zao za simu na kuacha mazoea ya kusubiri dakika za mwisho kuepuka msongamano na usumbufu mwingine unaoweza kujitokeza.

Aliuagiza pia uongozi wa Nida mkoa kusogeza huduma zake kwenye maeneo ya mkusanyiko wa watu ili waweze kuwafikia kwa urahisi . Alisema hali ya kufanya kazi kwa mazoea itasababisha kazi hiyo ya usajili isiende vizuri.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

1 Comments

  • avatar
    dotto fumba
    16/09/2019

    kwa wale ambao vitambulisho vyao vipo tayari natumeviona internet je tunaweza kuja kuijia kweny ofsini za nida ambapo tulipo andikishia au utaratibu upoje

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi