loader
Picha

Mabondia, wanamieleka kuchuana leo

MABONDIA wa ngumi za kulipwa, wa ridhaa na wanamieleka wanatarajiwa kuchuana leo kwenye ulingo mmoja katika pambano la kuwania mkanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Pambano hilo litapigwa kwenye klabu 361 Mwenge na kuwakutanisha mabondia raia na wanajeshi wanaozitumikia timu za taifa na jana walipima uzito tayari kwa mchuano huo mkali.

Kwa upande wa ridhaa, bondia mwanajeshi mkongwe, Selemani Kidunda atachuana na Amour Shehe kwa ajili ya kujiimarisha kuelekea michuano ya dunia ya majeshi inayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Kidunda alisema, “Nimejiandaa vizuri dhidi ya mpinzani wangu, awe makini kwasababu niko vizuri. Hii ni mechi itakayoniweka vizuri kabla sijaelekea China katika mashindano ya Majeshi.”

Kwa upande wa mabondia wa ngumi za kulipwa wanaogombea mkanda ni Nassibu Ramadhan dhidi ya Issa Nampeche raundi 10 ambapo mshindi atapata mkanda huo.

Ramadhan alisema amejiandaa kushinda na kwamba atampiga mpinzani wake mpigo wa kibaba kwani huko nyuma walipowahi kukutana alikuwa mdogo ila sasa amekuwa huku Nampeche akisema mengi atazungumza kwa vitendo ulingoni.

Rais wa Chama cha Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO), Ustadh Yassin Abdallah aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kuwaunga mkono akiwemo Smart Gin na Kampuni ya bima ya Resulution.

Alisema mbali na mabondia hao kuna wengine 10 watachuana wakiwemo wanawake na kuwahimiza mashabiki mbalimbali wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi