loader
Picha

Mtoto - Niliangukiwa na watu walioungua

MAJERUHI wa ajali ya moto mkoani Morogoro wanatimiza siku 15 leo baada ya kutokea kwa tukio hilo Agosti 10, mwaka huu, huku mwanafunzi Mfaume Mrisho (13) akieleza namna alivyoparamiwa na kuunguzwa moto.

Mwanafunzi huyo wa Darasa la Sita katika Shule ya Msingi ya Mafisa A katika Manispaa ya Morogoro, alieleza namna alivyoungua moto huo ni kutokana na kuangukiwa na watu wawili waliokuwa wanakimbia huku wakiwaka moto baada ya lori aina ya Scania lililobeba mafuta ya petroli na dizeli kupinduka na kulipuka moto.

Lori hilo lenye namba za usajili T 717 DDF lenye tela namba T 645 CAN lilipinduka Agosti 10, mwaka huu eneo la Mzambarauni karibu na stendi ya Msamvu Manispaa ya Morogoro, barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro.

Majeruhi hao wakizungumza na gazeti hili juzi wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa akiwemo na mwanafunzi huyo, walisema walikumbwa na janga la kuungua moto kutokana na kuparamiwa.

Walisema idadi kubwa ya watu waliokuwa wakikimbia ovyo ambao nguo zao zililowa na mafuta ya petroli ambazo zilishika moto uliokuwa ukiwaunguza huku wakiwakimbilia watu kutaka wawasaidie kuwaokoa na kifo.

Mfaume alisema siku ya tukio asubuhi alikuwa anajiandaa kwenda kujisomea na alisikia kishindo cha gari kuangua na alioona ni gari la mafuta ambayo yalikuwa wakimwagika chini.

“Muda wa nusu saa kupita kishindo kikasikika na moto kuwaka na watu waliokuwa eneo hilo ukawafuata na wengine walikimbia huku wakiunguzwa na moto. Mimi nikiwa mbali na eneo hilo nami niliamua kukimbia, lakini niliangukiwa na mtu mmoja ambaye alikuwa akiungua moto kutokana na nguo zake kuwa na mafuta.

“Niliinuka kukimbia tena, lakini mwingine aliniangukia tena na moto ukaniunguza mkononi, shingoni na mgongoni na kupata majereha,” alieleza mwanafunzi huyo.

Alisema baada ya kuunguzwa moto sehemu ya mwili wake, alikimbilia kwanza nyumbani kwao na kumkuta mama yake mdogo ambaye alikopa fedha kumkimbiza katika zahanati binafsi ili kupatiwa matibabu.

“Mama yangu mzazi asubuhi hiyo alikwenda sokoni, na aliporudi na kuona hali hiyo alinipeleka zahanati binafsi iliyopo karibu na nyumbani, lakini wao walisema nipelekwe Kituo cha Afya Nunge, na hapo pia wakasema nifikishwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kuweza kutibiwa,” alisema Mrisho na kuongeza kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vyema baada ya kupatiwa matibabu tangu alipofikishwa hapo.

Naye Usenga Rajabu (40), alisema kabla ya lori hilo kuwaka moto alipita kwa kukanyaga kwenye eneo la mafuta yaliyosambaa ili kuvuka upande wa pili wa lami karibu na msikiti. Hata hivyo, alisema ghafla alisikia mlipuko wa moto na baadhi ya watu waliokuwa karibu na lori hilo wakiunguzwa na moto ambao baadhi walikuwa wakikimbia ovyo katika eneo.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi