loader
Dstv Habarileo  Mobile
Halmashauri Bumbuli hatarini kufutwa

Halmashauri Bumbuli hatarini kufutwa

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Vedasto Ngombale amesema hatua ya Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga, kushindwa kukusanya mapato kwa kiwango cha kutosha, kunaiweka katika hatari ya kufutwa.

Ngombale ameyasema hayo wakati wa kutoa maagizo kwa viongozi wa halmashauri hiyo, baada ya kupitia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

“Baada ya kupitia hesabu zenu za mwaka wa fedha 2017/2018, Kamati haijaridhishwa na hesabu zenu kwa sababu mmeshindwa kujibu hoja za ukaguzi.

“Pia mmeshindwa kusimamia Sheria ya Fedha na makusanyo yenu yako chini sana na hii inaweka ushawishi wa kutaka kuifuta Halmashauri ya Bumbuli ambayo ilianzishwa ili kusogeza huduma kwa wananchi, hivyo mkajipange kuongeza ukusanyaji wa mapato hadi kufikia asilimia 80” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Ngombale alimuagiza Mkurugenzi wa hamashauri hiyo kuitisha kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani ili kuwachukulia hatua za kinidhamu na kuwashusha vyeo watendaji wa halmashauri hiyo, ambao wameshindwa kuwajibika.

Pia Kamati hiyo imeuagiza uongozi wa Hamashauri ya Bumbuli, kuhakikisha inajibu hoja za ukaguzi na kuziwasilisha ofisi ya CAG kabla ya Septemba 30, mwaka huu.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi