loader
Picha

Mwili wa shujaa Mugabe kurejeshwa Jumatano

MWILI wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe (95) unatarajiwa kuwasili nchini humo keshokutwa. Mugabe alifariki dunia mwishoni mwa wiki nchini Singapore, ambako alikuwa akipatiwa matibabu tangu Aprili mwaka huu.

Akizungumza kijijini anakotoka kiongozi huyo Mashonaland, binamu wa Mugabe, Leo Mugabe ambaye pia ni Msemaji wa Familia hiyo, alisema kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo ndege iitakayobeba mwili wa mwanasiaa huyo, itaondoka Zimbabwe leo kwenda Singapore.

“Kule Singapore wanauandaa mwili. Na sasa tunachagua watu watakaokwenda kuuchukua, lakini kwa muda ulivyo mwili utawasili hapa nchini siku ya Jumatano (keshokutwa),” alisema Leo. Leo alieleza kuwa mpaka sasa familia hiyo, inajadili eneo ambalo kiongozi huyo atazikiwa.

“Suala la wapi atazikiwabado halijapata muafaka, ila kesho (leo) tutakutana na watu wa itifaki ili kujadili kwa kina suala hili,” alisisitiza. Mugabe aliyeongoza taifa kwa takribani miaka 39, ametajwa kuwa ni shujaa wa taifa hilo la Zimbabwe.

Kwa mujibu wa mila na tamaduni za Zimbabwe, ni kawaida kwa shujaa wa taifa kuzikwa katika eneo maalumu la mashujaa jijini Harare. Hata hivyo, serikali huruhusu familia kuchagua eneo la kuzikiwa ndugu yao.

MAMLAKA ya Maji ya Makonde iliyopo wilayani Newala mkoani Mtwara, ...

foto
Mwandishi: HARARE, Zimbabwe

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi