loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

MABUNGE MADOLA YAIBANA AFRIKA KUSINI KUBAGUA WAGENI

CHAMA cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) kimeibana serikali ya Afrika Kusini, kikiitaka iwalinde raia wa mataifa ya Afrika wanaoshambuliwa, kuuawa na kuharibiwa mali katika mashambulizi ya kibaguzi.

Msimamo huo wa CPA ulitangazwa bungeni jana na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alipozungumzia maazimio ya Mkutano wa Mabunge wanachama wa CPA uliomalizika Zanzibar hivi karibuni.

Ndugai alisema wanachama na washiriki wa mkutano huo aliosema umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya washiriki kuliko miaka mingine, wamesaini azimio maalumu kuhusiana na msimamo wao huo.

“Tumesaini andiko la pamoja lenye tamko ya kulaani na kupinga mauaji yanayofanyika Afrika Kusini yanayojulikana kama Xenophobia (Ubaguzi kwa wageni). Tumepinga vikali ukatili huu unaofanywa kwa Waafrika wenzetu.

Tumewataka viongozi wa serikali ya Afrika Kusini kuchukua hatua za haraka za kuwalinda raia wa kigeni kutoka mataifa ya Afrika,” alisema Ndugai. Alieleza kuwa jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa raia hao wa Afrika Kusini hawaui wazungu, wala wahindi au wageni wengine weupe bali walengwa ni waafrika.

“yaani waafrika sasa tunauana wenyewe kwa wenyewe,” Alisema ukatili na unyama unaoendelea kufanywa na raia hao wa Afrika Kusini hauwezi kuachwa ukaendelea kuota mizizi na ndio sababu wabunge wa CPA wameamua kufikisha andiko lao kwa viongozi wa Afrika Kusini.

WATOTO 84,625 waliokuwa na utapiamlo mkali, wametibiwa kuanzia mwanzoni mwa ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi