loader
Ramos amwita Pogba Madrid

Ramos amwita Pogba Madrid

WACHEZAJI kama nyota wa Manchester , Paul Pogba, mara zote wanakaribishwa Real Madrid, kwa mujibu wa nahodha wa Blancos, Sergio Ramos.

Pogba ametumia karibu msimu huu mzima kuhusishwa na kutaka kuondoka kwa Mashetani Wekundu, huku miamba hiyo ya Hispania ikitajwa miongoni mwa inayo muwania.

Matokeo yake, Pogba amebaki, lakini haitashangaza kuona tena Madrid ikihusishwa na nyota huyo wa Ufaransa katika usajili ujao. Na Ramos hana tatizo na hilo, akisema klabu hiyo mara zote iko tayari kukaribisha wachezaji aina ya Pogba.

“Nadhani Real Madrid mara zote milango iko wazi kwa wachezaji wazuri kama yeye (Pogba),” alisema Ramos alipozungumza na Express.

Ramos alikwenda mbali zaidi kuzungumzia kiwango cha mchezaji huyo akiwa Juventus na United. “Kwangu, Pogba ni moja kati ya wachezaji wazuri,” alisema Ramos.

“Yuko tofauti na ameonyesha thamani yake alipokuwa Juventus na sasa Manchester United.” Pogba kwa sasa nimajeruhi hali inayoipa wasiwasi United baada ya kukosa mechi ya Ufaransa dhidi ya Albania na Andorra.

United inatarajia Pogba atarejea akiwa fiti kwa ajili ya michezo inayofuata. Kikosi hicho kitarejea kwenye Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Leicester City kwenye uwanja wa Old Trafford, ikifuatiwa na mechi dhidi ya Kazakh Club Astana kwenye Ligi ya Europa Alhamisi ijayo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4269c12f83060843f91d2f8e487da936.jpg

CHAMA cha Makocha wa Ligi Kuu England ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi