loader
Dstv Habarileo  Mobile
Queen Latifah atoa neno kwa Nicki Minaj

Queen Latifah atoa neno kwa Nicki Minaj

TAARIFA za rapa, Nicki Minaj, kutaka kustaafu kufanya muziki zinazizima duniani kote, huku wadau wengi wakitoa maoni yao kuhusiana na tamko hilo alilolitoa hivi karibuni.

Queen Latifah (pichani) ambaye ni kati ya marapa bora wa kike wa muda wote alihojiwa na mtandao wa TMZ kuhusiana na anachokiona kutokana na uamuzi huo wa Nicki, ambapo kwa upande wake alibariki uamuzi huo na kusema haoni cha kupinga kutokana na ukweli kuwa Nicki amefanya makubwa kupitia muziki wake.

“Kama ni kweli ameamua kufanya hivyo tu- muache afurahie kile alichoamua. Tumuache apumzike kwa amani na upendo kwani amefanya makubwa mno katika muziki,” alisema Latifah, lakini akasisitiza kuwa ana amini mwanadada huyo ipo siku atarejea tena katika tasnia hiyo.

“Lakini niwaambie kitu kimoja kama uliwahi kuwa rapa basi utabaki kuwa hivyo kwa miaka yote. Ipo siku atarudi tu, mwacheni kwanza aishi maisha yake kwa sasa kwa upendo na amani aliyoichagua,” alisema Latifah huku akitabasamu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d74e35a91a2a38780d1ea458f291fba2.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi