loader
Picha

Queen Darleen akana ujauzito

MSANII Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’ amekana taarifa kuwa ni mjamzito na kushangaa tetesi hizo zilivyoanza mpaka kufi ka kwake hali ya kuwa ahusiki na jambo hilo.

Mwezi mmoja sasa umepita tangu zilipoanza tetesi hizo ambapo baada ya kupata taarifa hizo alikanusha mbele ya waandishi wa habari na kuwataka wamwangalie vizuri kama ni mjamzito.

“Hiyo ni mitandao tu sio kweli, stori za kutunga hizo, hebu niangalie vizuri kwa ukaribu niangalie unaona ujauzito wowote hapo,” alihoji Queen Darleen.

Msanii huyo ambaye ni mwanachama wa WCB alikanusha pia kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Lukamba ambaye ni mpigapicha wa Diamond na kwamba ni kaka yake wanafanya kazi pamoja.

Queen Darleen kwasasa anatamba na wimbo wake wa Mbali alioshirikiana na Harmonize ambao umeendelea kufanya vizuri hasa kwenye mtandao wa Youtube.

MABINGWA wa kihistoria Yanga kupitia Kampuni ya GSM wamesema wanajipanga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi