loader
Mohammed Mdose

Mohammed Mdose

LEO Timu ya soka ya taifa, Taifa Star itashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuwakaribisha Sudan katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na historia ya timu hizo ambapo mwaka 2008 Tanzania iliitoa Sudan na kufuzu fainali za Chan zilizofanyika kwa mara ya kwanza 2009 Ivory Coast.

Baada ya mchezo wa leo timu hizo zinatarajiwa kurudiana katikati ya mwezi ujao na mshindi wa jumla atakata tiketi ya moja kwa moja kushiriki fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika Cameroon, mwakani kati Januari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kocha Msaidizi wa taifa Stars, Juma Mgunda alisema kuwa wana kila sababu ya kupata ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu.

Alisema wamekuwa na matokeo yasiyoridhisha ndani ya dakika 90 jambo ambalo limekuwa likiwaumiza kichwa na wamelifanyia kazi na wanaamini wameshalimaliza.

“Najua mechi zetu zilizopita kuna mazuri yalionekana na mapungufu yalionekana, benchi la ufundi limeyafanyia kazi kikamilifu kwa program maalumu naamini tumeyamaliza na kama Mwenyezi Mungu akitujaalia tutafanya vizuri.

“Niwahakikishieni kazi tumeifanya na tutahakikisha tunafanya vizuri katika mechi ya kesho na kazi hiyo itaonekana,” alisema Mgunda.

Nae kocha mkuu wa Sudan, aliyewahi kuinoa Simba SC, Zdravko Logarusic, alisema kuwa ameiona Tanzania katika mechi zake kadhaa zilizopita na kugundua kuwa ni moja kati ya timu ngumu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Alisema, anakumbuka kuwa Tanzania ndio waliwafanya wasishiriki fainali za mwaka 2008 wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufanywa ngazi na Taifa Stars na kukata tiketi 2009 hivyo wamejipanga kulipa kisasi.

“Tumejiandaa kukabiliana na timu ya Taifa ya Tanzania, tumeiona katika mechi zao zilizopita ni timu ambayo ukikutana nayo inakupa changamoto nyingi ina makocha wapya ambao wanaijenga timu siku hadi siku, hatutaweza kuwadharau katika mechi ya kesho (leo) tutaingia kwa kutafuta matokeo,” alisema Logarusic.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a7891ff5483db9b488f6b4c20f436b6d.jpg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Sudan hatoki Taifa leo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi