loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pongezi ATCL kufikia asilimia 75 ya soko

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza nafasi za wauza tiketi, ofi sa masoko ya biashara ya mtandao na pia wale wa mizigo. Imetoa tangazo hilo siku chache baada ya Rais John Magufuli kuisifu kwa kufanikiwa kuhodhi asilimia 75 ya soko la usafiri wa anga nchini.

Akizindua rada mbili za Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA), Rais Magufuli alisema ATCL inajitanua kibiashara ikipanga kuongeza ndege hadi 11 na safari za China.

Naungana na Rais Magufuli kuipongeza ATCL kwa mafanikio inayopata. Ni matarajio yangu itazidisha juhudi kusimamia vizuri kampuni. Ifanye hivyo ikijua imani kubwa, ambayo jamii inayo kwake kufuatia mageuzi na uwekezaji huu mkubwa, ambao Rais Magufuli anaifanyia sasa.

Wakati huu ambapo rada mbili zimezinduliwa, iko haja ATCL kuboresha huduma ziwe nafuu. Hivi karibuni wataalam wa usafiri wa anga Uganda, walipendekeza nauli za ndege Afrika Mashariki zitozwe nafuu kama safari za ndani. Wazo hili zuri linalenga kuziwezesha ATCL, Kenya Airways ya Kenya, Uganda Airways ya Uganda na Rwandair ya Rwanda, kutoza nauli nafuu zaidi kwa abiria wa ukanda huo ili wengi wapande.

Moja ya sababu za abiria wengi hukwepa ndege ni nauli ghali, ambayo ni Sh. 200,000 na zaidi. Kwa wengi nauli hiyo imeonekana ni kubwa mno. Uzoefu unaonesha abiria wa Kanda ya Ziwa, wanatamani nauli ya ndege isizidi Sh.100,000.

Iko haja kwa ATCL kuangalia eneo hilo kwa umuhimu mkubwa, ikibidi kuomba serikali ili baadhi ya kodi zipungue abiria zaidi wapande. Ikibidi itafutwe njia kuipunguzia ATCL mzigo, kwa kupunguza tozo za kutumia viwanja vya ndege kwa kuiwezesha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwa na miradi.

TAA hutoza ndege kama moja ya vyanzo vya mapato upande wa ndani wa uwanja, na hukodisha maeneo ya hoteli na maghala upande wa nje. Ni muhimu TAA ikawezeshwa zaidi miradi ya upande wa nje ili ipunguze tozo kwa ATCL, angalau safari za ndani wengi wafaidi ndege.

Pia ATCL iangalie soko la ndege ndogo za kukodi kwa ajili ya watalii, kwani ni moja ya eneo linaloonekana kufanya vizuri sekta binafsi. Hii itasaidia ndege ndogo, kuleta abiria kutoka viwanja vidogo zaidi, kuunganisha Bombardier na Airbus au Dreamliner, kwa wanaoenda nje.

Nasema haya nikirejea uzoefu nilioupata nikiwa Ofisa Uhusiano/ Sheria TAA nilipozungumza na marubani wa ndege ndogo binafsi za kukodi.

Marubani walionesha uwepo wa fursa zaidi viwanja vya pembezoni, baada ya kwenda huko kukimbia ndege kubwa zilizotawala soko la viwanja vikubwa vinavyojengwa kuboreshwa.

Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, ...

foto
Mwandishi: NA GODFREY LUTEGO

1 Comments

  • avatar
    Morgan shayo
    23/09/2019

    Naulizia nafasi za kazi yoyote ile.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi