loader
Picha

KUBORESHWA KWA MALIPO YA FIDIA KWALETA FARAJA KATIKA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

Tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa uking’ara kwa utoaji wa huduma bora nchini. Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015].

Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kulipa fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Sambamba na huduma bora, wadau mbalimbali wameendelea kushuhudia WCF inavyoleta faraja kubwa kwa wafanyakazi na kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro kati ya waajiri na wafanyakazi kutokana na maboresho ya huduma za fidia kwa wafanyakazi tangu Mfuko ulipoanza kupokea madai Julai Mosi, 2016.

Kabla ya kuanzishwa kwa WCF, viwango vya fi dia kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na umma vilikuwa vidogo sana na malipo hayo yalilipwa kwa mkupuo yaani mara moja (lumpsum) kwa wafanyakazi wa sekta zote hata kama ajali ilipelekea kifo.

Mathalani kiwango cha juu cha fi dia kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kilikuwa TZS. 108,000/= wakati kima cha juu kwa wafanyakazi wa sekta ya umma kilikuwa TZS. 12,000,000/=.

Hali ilikuwa ngumu zaidi kwa wategemezi wa wafanyakazi waliopata ulemavu wa kudumu au kifo kwa sababu ya kutokuwepo kwa malipo ya fi dia endelevu (pensheni). Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Masha Mshomba, anabainisha kuwa ‘’kwa sasa endapo mfanyakazi ataumia au kuugua na kupata ulemavu wa kudumu wa asilimia mia moja (100%), WCF itamlipa Mfanyakazi huyo fidia ya asilimia sabini (70%) ya mshahara wake kila mwezi kwa maisha yake yote’’.

Mshomba anaendelea kufafanua kuwa WCF inatoa mafao mbalimbali kwa mfanyakazi aliyeumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.

Mafao hayo ni pamoja na huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, malipo kwa wategemezi iwapo mfanyakazi atafariki, msaada wa mazishi pamoja na huduma za utengemao.

Kuhusu huduma ya matibabu na utengemao, Mshomba anaeleza kuwa WCF imeingia mikataba na taasisi mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na hospitali mbalimbali zikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Hospitali ya Benjamin Mkapa - Dodoma, Hospitali ya KCMC - Moshi, Hospitali ya Seliani (Arusha Lutheran Medical Centre, Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Hospitali ya Rufaa ya St. Francis Ifakara, Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Hospitali ya Mount Meru, Arusha, Hospitali ya CCBRT, Hospitali ya Dar Group, Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na Hospitali ya Kanda ya Mbeya.

“Kwa sasa wagonjwa wenye maradhi au waliopata ajali kutokana na kazi wanapokelewa na kuhudumiwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizo katika sehemu mbalimbali nchini” anaeleza Mshomba.

Akitoa takwimu za ulipaji wa fi dia, Mshomba anasema malipo ya fi dia nchini kwa mwaka mzima yalikuwa chini ya shilingi milioni 200 kabla ya kuanzishwa kwa WCF lakini baada ya kuanzishwa kwa Mfuko huu malipo yanaongezeka mwaka hadi mwaka.

Mshomba anafafanua kuwa hadi kufi kia mwisho wa mwezi Juni 2019, Mfuko ulikuwa umefanya malipo ya mafao kwa wanufaika takribani 2,308 na kiasi cha takribani shilingi bilioni 7.90 kililipwa.

Aidha, malipo endelevu ya kila mwezi (Pensheni) yanaendelea kulipwa na kiasi cha shilingi milioni 52.95 zililipwa kwa wanufaika 187 katika mwezi Juni 2019.

Sambamba na ulipaji wa mafao bora, Mshomba anabainisha kwamba Mfuko umepata mafanikio makubwa katika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma kupitia utumiaji wa mifumo ya kielekroniki (TEHAMA), kuimarika kwa tathmini za ajali na magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na usogezaji wa huduma kwa wadau.

Mshomba anaeleza kuwa kwa sasa wadau wa Mfuko ambao wanatumia huduma za mtandao hawalazimiki kufi ka ofi sini ili kupata huduma za fi dia.

Anasema kuwa WCF imetoa fursa kwa wateja wake kupata huduma mbalimbali kupitia mifumo ya kielektroniki (TEHAMA) iliyoboreshwa.

Baadhi ya mifumo ya kielektroniki iliyosimikwa ni pamoja na Mfumo wa Usajili wa Waajiri ambao unamwezesha Mwajiri kujisajili (online registration) na kupata hati ya usajili kwa kutumia muda wa takribani dakika tano bila kufi ka katika ofi si za Mfuko, Mfumo wa uwasilishaji wa michango ambao unamwezesha mwajiri kutunza taarifa za wafanyakazi na kuwasilisha michango kupitia nambari ya udhibiti (control number) na kupata stakabadhi ya kielektroniki pamoja na Mfumo wa uwasilishaji wa taarifa za tukio la ajali, ugonjwa na kifo ambao unamwezesha mwajiri kutoa taarifa ya tukio kwa wakati, kuwasilisha nyaraka na kujua hatua iliyofi kiwa katika uchakataji wa madai kwa njia ya mtandao.

Pamoja na hatua kubwa ambayo Mfuko umepiga katika utoaji huduma za mtandao, Mfuko umejizatiti kuendelea kuboresha mifumo yake ya kielekroniki kwa kuwezesha huduma zote kutolewa kwa njia ya kieletroniki kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo mpango mkakati wa kwanza wa Mfuko utamalizika.

Mpaka sasa matumizi ya TEHAMA yamefi kia asilimia 65%, anaeleza Mshomba. Akiendelea kufafanua zaidi, Mshomba anaeleza kuwa mifumo hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa usumbufu uliokuwepo awali kwa waajiri na wawekezaji nchini katika kujisajili na kupata huduma mbalimbali za Mfuko.

Kwa sasa, waajiri wote wanaweza kupata huduma hizi wakiwa katika mkoa wowote nchini bila kulazimika kwenda moja kwa moja katika ofi si za Mfuko. “Katika kuhakikisha wadau wetu wanashiriki kimamilifu kwenye mnyororo wa thamani wa utoaji wa huduma bora kwa umma, Mfuko umeendelea kuwajengea uwezo madaktari nchi nzima hasa katika ufanyaji tathimini za magonjwa yatokanayo na kazi.

Hadi kufi kia tarehe 31 Agosti, 2019 takribani madaktari 856 walikwishapatiwa mafunzo maalumu kuhusu tathmini za ulemavu utokanao na ajali pamoja na magonjwa yatokanayo na kazi” anasema Mshomba. Mshomba ameahidi kwamba,

Mfuko utaendelea kutoa mafunzo hayo kwa madaktari nchini kwa kutumia wataalamu wa ndani ya Mfuko kwa kushirikiana na taasisi wadau zikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Kuhusu chachu ya mafanikio ya Mfuko, Mkurugenzi Mkuu ameeleza kuwa msaada mkubwa wa Serikali pamoja na ushirikiano kati ya WCF na wadau mbalimbali umekuwa ni nguzo kubwa.

Wadau hawa ni pamoja na Waajiri, Wafanyakazi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Chama cha Waajiri (ATE) na Shirika la Kazi Duniani ILO. Kwa upande wa Serikali, WCF imeendelea kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wizara na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofi si ya Waziri Mkuu, (Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu), Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha na Mipango, Ofi si ya Rais (Utumishi), Ofi si ya Rais (TAMISEMI), Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) pamoja na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini) GPSA).

Mnamo tarehe 27 Mei 2019, WCF na Mfuko wa Fidia wa Zambia (WCFCB) walisaini mkataba wa ushirikiano utakaosaidia kubadilishana uzoefu katika nyanja za ulipaji mafao ya fi dia kwa matukio ya ajali, magonjwa ama vifo vitokanavyo na kazi.

Aidha, mwezi Agosti 2018, WCF ilisaini makubaliano ya ushirikiano kati yake na Mfuko wa Fidia wa Ujerumani (DGUV) ambapo pamoja na mambo mengine, makubaliano haya yanatoa nafasi kwa Tanzania kujenga uwezo zaidi katika utoaji wa huduma za fi dia pamoja na kupata misaada mingine ya kitaalamu.

Sekta ya viwanda ni moja kati ya sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa taifa na maendeleo ya jamii. Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayojenga uchumi wa viwanda, Mshomba anasema Mfuko umejiandaa kikamilifu katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda.

Kwa sasa, Mfuko kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaendelea na hatua za kuwekeza katika kiwanda cha vifaa vya tiba mkoani Simiyu.

Pamoja na mambo mengine, uwekezaji katika viwanda unalenga kuongeza fursa za ajira nchini ili kufi kia uchumi wa kati ifi kapo mwaka 2025, anaeleza Mshomba.

Akizungumzia huduma zingine zitolewazo na WCF, Mshomba anabainisha kwamba Mfuko umeendelea kufanya maboresho makubwa ili kukidhi mahitaji halisi ya wadau wao. Anaeleza kuwa katika kipindi cha muda mfupi yaani kipindi cha miaka minne tangu kuanzishwa kwa Mfuko huu, WCF imefanikiwa kusogeza huduma za fi dia kwa wadau kwa kufungua ofi si za kanda nchini.

Akitaja Ofi si hizo, Mshomba anasema kuwa kwa Kanda ya Kati ofi si zinapatikana Dodoma, Barabara ya Jakaya Kikwete, Kitalu Na. 1 na 2, Jengo la PSSSF Plaza; Kanda ya Pwani Ofi si zinapatikana Dar es Salaam, Barabara ya Bagamoyo, Mtaa wa Regent, Kitalu Na. 37, jengo la PSSSF, Ghorofa ya Chini na ya 6; Kanda ya Kaskazini, ofi si za WCF zinapatikana Arusha, jengo la Idara ya Kazi; Kanda ya Ziwa, Ofi si zinapatikana Mwanza jengo la Idara ya Kazi, Barabara ya Stesheni mkabala na Lake Hotel; na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ofi si zinapatikana Mbeya jengo la NHIF, Kitalu Na. 3, Barabara ya Karume.

Aidha, anaeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2019/20, WCF imekusudia kuongeza ofi si za mikoa katika mkoa wa Mtwara, Tabora, Geita na Morogoro. Mshomba anaendelea kueleza kwamba katika miaka minne tangu kuanzishwa kwake, WCF imeendelea kutekeleza Ilani ya chama tawala, hususani katika kupunguza umaskini kufuatia mafao bora yanayotolewa kwa wanufaika.

Aidha, WCF imechangia kwa kiasi kikubwa katika kupanua wigo wa hifadhi ya jamii kwa Watanzania. Yote haya ni sehemu tu ya mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, imeleta na inaendela kuleta kwa wafanyakazi na Watanzania wote kwa ujumla.

‘’WCF tutaendelea kutoa huduma bora ili kuwa mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma za fi dia kwa wafanyakazi barani Afrika kwa lengo la kupunguza athari za kijamii na kiuchumi kwa wafanyakazi, familia zao na waajiri mara baada ya kuumia au kuugua kazini’’, anahitimisha Mshomba.

WAKULIMA wa Kijiji cha Manda Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ...

foto
Mwandishi: Na. Laura Kunenge

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi