loader
Simba yaitwanga Kagera

Simba yaitwanga Kagera

SIMBA imeendokana na jinamizi lililokuwa likiwaandama kwa muda mrefu baada ya jana kuifungasha timu ya Kagera Sugar mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mchezo huo ulianza kwa kasi na hali ya utulivu wakati wenyeji Kagera wakionekana kujiamini vya kutosha na kumiliki eneo la katikati kwa dakika za mwanzo na wapinzani wao Simba walionesha utulivu mkubwa hasa katika safu ya ulinzi.

Dakika ya nne ya mchezo, Simba ilifanya shambulizi la kushtukiza baada ya mabeki wa Kagera kujisahau na mshambuliaji Meddie Kagere kutundika bao la kwanza la kichwa akitumia vyema pasi iliyopigwa na Deogratius Kanda.

Baada ya kupata bao hilo, Simba iliendelea kucheza kwa kutulia, licha ya kuzidiwa eneo la kati kwa dakika hizo, huku ikitumia mipira ya pembeni, ambayo ilikuwa na faida kwa kaisi kikubwa baada ya beki Mohammed Hussein kutundika bao la pili akitumia pasi ya Meddie Kagere.

Kipindi cha pili kilianza kwa Kagera kupitia eneo la kati la viungo lakini wapinzani wao walikuwa imara katika eneo hilo, hivyo walilazimikan kubadili kwa dakika kadhaa na kuanza kutokea pembeni ambako hata hivyo hawakufanikiwa.

Wakati Simba ikiongoza mabao mawili, dakika ya 71, kiungo Ibrahim Ajib ambaye alikuwa na mchezo mzuri alitolewa baada ya kupata maumivu ya mdomo na na- fasi yake kuchukuliwa na Hassan Dilunga, ambaye dakika 78 alikosa bao la wazi.

Simba ilifanya mabadiliko mengine winga Deo Kanda alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Miraj Athuman aliyekuwa na mchezo mzuri baada ya kusababisha penalti dakika ya 77 iliyozaa bao la tatu la Kagere, hivyo kufikisha mabao matano katika msimamo wa Ligi.

Matokeo hayo yamefanya Simba kuondokana na lile jinamizi lililokuwa likiwasumbua kwa muda mrefu wanapokutana na Kagera Sugar, kwani ndani ya msimu miwili Simba haikuwahi kupata matokeo ya ushindi dhidi ya timu hiyo.

Nahodha wa timu hiyo, Mohammed Hussein alisema walitambua kuwa Kagera siyo timu ya kubeza hivyo walijipanga ili kuendelea na rekodi yao ya ushindi waliyoianza msimu huu, ambapo mpaka sasa hawajafungwa wala kutoa sare.

“Tunashukuru Mungu tumeshinda, tumecheza kwa kujituma maana tunajua matokeo yaliyopita yalinyokuwa kwa hiyo binafsi nimejisikia furaha kwa kuwafunga pia,”alisema Mohammed Hussein.

Katika mchezo wa mwisho wa Ligi, Simba ilipoteza kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru msimu uliopita dhidi ya Kagera Sugar.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4b4b0bb12f7b25b1a56d8e56ae149222.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi