loader
Magari 78 yanaswa kutumia barabara za mwendokasi

Magari 78 yanaswa kutumia barabara za mwendokasi

WAKATI Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimwagiza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Marison Mwakyoma kuwakamata madereva wanaotumia barabara za Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (UDART) maarufu mwendokasi na kuwafi kisha katika vyombo vya sheria, tayari magari 78 yakiwamo ya taasisi za serikali yameshakamatwa.

Alitoa maagizo hayo Dar es Salaam jana wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la michoro ya alama za usalama barabarani, linaloendeshwa na Kampuni ya mafuta ya Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend.

Makonda alisema kumekuwa na tabia iliyozoeleka kwa watumiaji wa vyombo vya moto, kuzitumia barabara za mabasi yaendayo haraka kiholela jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na kusababisha ajali za mara kwa mara ambazo zingeweza kuzuilika.

Alisema ameshangazwa kuona bado watumiaji wa vyombo vya moto wanaendelea kuzitumia barabara hizo bila ya woga, licha ya kutolewa kwa maagizo mara kwa mara na viongozi wakuu jambo ambalo limesababisha kutokea kwa ajali za mara kwa mara baina ya mabasi ya mwedokasi na vyombo vingine vya moto.

“Nimepita hapa Kariakoo kwenye mwendokasi hali sio nzuri. Watembea kwa miguu wapo kwenye mwendokasi, wanaotumia magari wanatumia mwendokasi ambao sio barabara yao. Kwa hiyo wewe uliyepo hapa (Afande Swai) mwambie Afande Mwakyoma kabla sijaondoka hapa nikute kuna trafiki wanaokamata watu wanaotumia hiyo barabara kwa matumizi yao tofauti na makusudio,” alisema Makonda.

Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, kuendesha operesheni maalumu Kariakoo kuanzia Faya mpaka Gerezani na kukamata vyombo vyote vya moto vinavyotumia barabara hiyo kinyume cha sheria.

Makonda alisema madhara yatokanayo na matumizi ya barabara hiyo ni makubwa hususani kwa watoto wadogo wanaosoma katika shule zilizopo Kariakoo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e7fe4b4bfea089664a1f9a0b08d6d424.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Na Fadhili Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi