loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bodaboda wapewa kofia ngumu

Bodaboda wapewa kofia ngumu

MADEREVA wa bodaboda kutoka kata nane za Manispaa ya Kinondoni wamepewa msaada wa kofia ngumu na Kampuni ya Mcheza ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa ya kujikinga na ajali za barabarani wao na abiria.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Biafra baada ya kukabidhiwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Bajaji na Bodaboda Kinondoni, Issa Mustapha alisema waliopewa kofia wengi ni viongozi wa vituo ambao pia ni madereva ili wakawe mfano kwa wenzao kuhamasisha kuvaa helmenti.

“Tulipewa kofia ngumu 100, tuna madereva wa bodaboda na bajaji 7,000 lakini kwa sababu kofia tulizopewa hazitoshi kwa wote tukaona tuwape viongozi baadhi wa vituo wakawe mfano kwa madereva wao wakiwa kazini,” alisema Mustapha.

Kwa upande wake, Balozi wa Mcheza, Edger Kibwana alisema huu ni utaratibu wao walioanzisha mwaka huu kuhakikisha usalama kwa madereva wa bodaboda unakuwa mkubwa sana wanapokuwa kazini kwa kuwapa vifaa hivyo vitakavyosaidia kutoa huduma bora kwa Watanzania.

“Tunawasihi bodaboda kuendelea kuzingatia sheria za usalama kama wanavyoelekezwa na serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, na sisi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha usalama wao unakuwa mzuri, M cheza ipo pamoja nao Watanzania waweze kunuifaka na huduma yao,” alisema Kibwana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Mcheza, Moses Busaimoni alisema utoaji wa kofia hizo ni kuunga mkono juhudi za vyombo vya usalama za kuelimisha umuhimu wa madereva na abiria kuvaa kofia ngumu kujiepusha na hatari ya kupoteza maisha pindi wanapopata ajali.

Alisema bado wataendelea kuwaunga mkono madereva hao ambapo hivi karibuni watakuja na shindano linalowahusu lenye lengo la kutoa zawadi za bodaboda kwenye kata mbalimbali.

“Nawakumbusha madereva wa bodaboda kuwa tumeandaa shindano dhidi yao washindi watanyakua bodaboda, wajiandae utaratibu tutauweka hadharani hivi karibu ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/088a9dc818458bd9dff9eb7cca8b4ec3.jpg

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi