loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima wa korosho, watumishi wa umma kicheko

KOROSHO yote tani 225,105 iliyonunuliwa na serikali kwa Sh bilioni 720 kutoka kwa wakulima wa zao hilo kwenye maghala mbalimbali nchini, imeuzwa katika soko la ndani na nje.

Tayari tani 98 zimeshaondoka kupita bandari ya Dar es Salaam na Mtwara ikiwa ni asimilia 41 ya korosho yote. Aidha, kati ya korosho hizo, jumla ya tani 211,587 zimeuzwa soko la nje ambapo wanunuzi 21 walijitokeza kuinunua huku meli kubwa iitwayo Christina ikitia nanga katika bandari ya Mtwara kwa ajili ya kupakia tani kadhaa kati ya tani 104 zinazosafirishwa kupitia bandari hiyo.

Wakati huo huo, kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, serikali imelipa jumla ya Sh bilioni 85.72 kwa watoa huduma, watumishi na madai mengine mbalimbali ikiwemo malimbikizo ya mishahara.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi alisema serikali imejipanga vizuri na inatekeleza ahadi yake ya kununua korosho yote ya wakulima iliyokuwa kwenye maghala mbalimbali nchini yaliyoidhinishwa kuhifadhi korosho hizo baada ya kuzinunua kwa bei ya Sh 3,100 baada ya wanunuzi kutaka kuzinunua kwa bei ya chini.

“Kwanza niwahakikishie wakulima wa korosho nchini kwamba serikali inapofanya jambo inatimiza, ilisema itanunua korosho zote za wakulima na imefanya hivyo, ingawa kuna changamoto za wakulima wachache ambao bado hawajapata fedha zao ila niwahakikishie kuwa malipo yao yanaendeleo kutolewa hata jana na leo malipo yanaendelea kufanywa,” alisema Dk Abbasi.

Akizungumzia korosho zilizouzwa ndani, alisema kati ya korosho zote tani 225,105 zilizonunuliwa na serikali tani 4,595 zimeuzwa kwenye soko la ndani na hadi kufikia Oktoba 20, mwaka huu korosho yote iliyobaki kwenye maghala itakuwa imeshaondolewa ili kupisha msimu mpya wa mavuno. Kuhusu madeni ya mbalimbali nchini, alisema kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, serikali imeshalipa jumla ya Sh bilioni 85.72 kwa watoa huduma, watumishi na madai mengine mbalimbali ikiwemo malimbikizo ya mishahara.

Alisema kati ya fedha hizo, Sh bilioni 50 zimelipwa kwa ajili ya kulipa madeni ya pensheni za watumishi, huku Sh bilioni 22 zikitumika kulipa madeni ya wastaafu 3,019 malimbikizo ya mishahara ya watumishi 1,435. Aidha, Sh bilioni 10.24 zimetumika kulipa madeni ya wazabuni ambao ni watoa huduma mbalimbali nchini na Sh bilioni mbili zimetumika kuwalipa wakandarasi waliotoa huduma nchini kwenye miradi tofauti.

Kuhusu malalamiko yanayoendelea kwenye kitandao ya kijamii kudai serikali imevunja Katiba kwenye suala la kesi za wahujumu uchumi, Dk Abbasi alitoa ufafanuzi na kusema serikali huwa haikurupuki kufanya jambo.

“Kwanza masuala ya kesi na DPP, tuwe makini nayo tusiingilie kesi zilizoko mahakamani, ila nitoe ufafanuzi wa kitaalamu kwenye hilo la Katiba, ni kwamba serikali haijakurupuka kumshauri DPP, kwa sababu kwa Mujibu wa Sheria mpya ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2019, kifungu 194 (A), kinatoa nafasi ya kushauriwa,” alisema Dk Abbasi.

KATIBU Tawala wa Wilaya ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi