loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Wakimbizi hawarudishwi Burundi kwa kulazimishwa’

SERIKALI imesisitiza kuwa suala la kuwarudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao sio la kulazimishwa, bali viongozi wa mataifa hayo mawili na raia hao, walikubaliana baada ya hali ya amani nchini humo kurejea.

Akitoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa Tanzania kuwarudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao kuanzia Oktoba Mosi, mwaka huu, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi alisema hakuna wahamiaji waliolazimishwa kurudi makwao, bali waliokubali kurejea ni wale tu walioamua wenyewe, baada ya hali ya amani nchini kwao kurejea.

“Kwanza hakuna wakimbizi waliolazimishwa na serikali ya Tanzania kurudi Burundi, kuna sheria na mikataba ya haki na kinga za wakimbizi ya kimataifa ambayo tumeifuata katika kuhakikisha wale wanaorejea kwao wanafika salama na kuendelea na maisha yao,” alisema Dk Abbasi.

Alisema Tanzania ni nchi inayoheshimu mikataba ya kimataifa na inajua haki na kinga za wakimbizi na kwamba hata kabla ya kuwepo kwa mikataba hiyo, nchi ilikuwa na utaratibu wa kuwapokea wakimbizi na kuwahifadhi na hilo halina ubishi.

Dk Abbasi alisema Burundi na Tanzania zilikubaliana mwezi Agosti mwaka huu, kuwa mchakato wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi zaidi ya 2,000 wa Burundi waliopo nchini Tanzania, utaanza Oktoba mosi.

Alisema hali ya Burundi kwa sasa ni ya amani na kwamba changamoto ndogo zilizopo, ziko kwa mataifa mengi Afrika, lakini sio kigezo cha wakimbizi kutorejea kwao. Kwamba katika kuwarejesha wanafuata miongozo. Awali,Waziri wa Maambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, Kangi Lugola alisema wakimbizi 2,000 wa Burundi watarejeshwa kwao kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi