loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jitokezeni kujiandikisha mchague viongozi

JANA Watanzania nchi nzima walianza kujiandikisha katika Daftari la Orodha ya Wapigakura kwa ajili ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.

Kanuni za uchaguzi zinabainisha kwamba uandikishaji na uandaaji wa orodha ya wapigakura kunafanyika siku 47 kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa siku saba kwa kutumia fomu maalumu.

Kwa mujibu wa Waziri mwenye dhamana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, undikishaji utafanyika katika majengo ya umma.

Jafo anasema na pale ambapo hakuna jengo la umma, uandikishaji utafanyika kwenye sehemu ambayo msimamizi msaidizi wa uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa vyama vya siasa.

Kwanza tunawakumbusha Watanzania wote kwamba uchaguzi huu ni muhimu sana kwa mustakabari wa maslahi mapana ya nchi. Tunaamini kila Mtanzania ni lazima aone umuhimu wa kujiandikisha ili atumie nafasi hiyo ya kipekee kumchangua kiongozi anayeona anafaa.

Lakini pia tuwakumbushe kwamba asiyejiandikisha katika daftari la orodha ya wapigakura, anakuwa umepoteza nafasi ya kuchagua kiongozi wake wa mtaa.

Ikumbukwe kwamba hivi sasa masuala yote ya kijamii kuanzia mikopo, safari, udhamini, na mengineyo yanaanzia kwenye Serikali za Mitaa, hivyo kuacha kujiandikisha na kukosa nafasi ya kuchagua kiongozi wa mtaa maana yake unajinyima haki ya kupata kiongozi bora na si bora kiongozi ambaye atakutumikia kwa kipindi chote cha miaka mitano ijayo.

Jafo anasema makisio ya kuandikisha wapiga kura kwa uchaguzi huu ni Watanzania 26,960,485 ambapo kati ya hao, wanaume ni 12,852,328 na wanawake ni 14,108,157 huku utaratibu wa kuandikisha wapigakura ulioanza jana, utafanyika kwa siku saba hadi Oktoba 14 mwaka huu.

Anasema katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, zaidi ya milioni 11.49 ikiwa ni asilimia 62 ya makadirio ya kuandikisha watu 18,587,742 walijiandikisha katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka 2014.

Akaongeza kwamba mikoa ya Katavi na Kagera ilifanya vizuri zaidi kwa kuandikisha kwa asilimia 79 na asilimia 78 katika uandikishaji huo huku mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro ikiwa imefanya vibaya kwa kuandikisha kwa asilimia 43 na asilimia 50.

Tunaipongeza mikoa hiyo lakini tunawakumbusha wananchi wa mikoa hiyo kwamba, mwaka huu wasilale kwani mambo yanabadilika, waliokuwa wa kwanza wasije wakajikuta wa mwisho na wa mwisho wakawa wa kwanza.

Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi