loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFF isiwatelekeze Vijana wetu wa U-20

TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania Bara chini ya miaka 20 (U-20), wiki iliyopita ilitwaa ubingwa wa michuano ya Cecafa kwa umri huo baada ya kuifunga Kenya kwa bao 1-0 katika fainali nchini Uganda.

Tanzania Bara, ambayo katika hatua ya makundi ilipangwa pamoja na Zanzibar, Kenya na Ethiopia, ilishinda mechi mbili na kutoka sare moja dhidi ya Kenya, ambayo walikuja kukutana nayo katika fainali ya michuano hiyo.

Timu hiyo ilionesha uwezo mkubwa wa kusaka kabumbu na hiyo sio kitu cha kubahatisha ila ilitoka na kukaa pamoja kwa muda mrefu huku wachezaji wengi walikuwa pamoja katika timu ya U-17, ambayo ilishiriki mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kupongezwa kwa kuijali timu hiyo pamoja na zingine za vijana, kwani msingi wa soka huanzia katika timu za vijana na baadaye huibukia kwa wakubwa.

TFF isiitelekeza timu hiyo ya U-20 pamoja na zingine za vijana kwani huo ndo utakuwa msingi mzuri wa timu zetu za wakubwa za Kilimanjaro Stars (Tanzania Bara) pamoja na ile ya Taifa Stars (Tanzania) katika mashindano ya kimataifa.

Pamoja na kuwa timu yetu ya U-17 haikufanya vizuri katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa umri huo mwaka huu yaliyofanyika nchini, lakini hilo lisitukatishe tamaa na badala yake ndio iwe chachu ya kuwekeza zaidi kwa vijana.

Timu nyingi za taifa au hata klabu zimefanikiwa kutokana na kuwekeza kwa soka la vijana mfano mzuri wa hivi karibuni kabisa ni timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya nchi hiyo ya Ajax, ambayo ilifikia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita.

Timu hiyo ya taifa pamoja na klabu hiyo, zote zime- kuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuwa na msingi mzuri katika soka la vijana, ambalo limerejesha heshima ya Uholanzi katika soka, ambayo miaka kadhaa iliyopita ilipotea kimataifa.

Ushauri wetu kwa TFF kuwa timu hiyo ya U-20 isitelekezwe na badala yake ishirikishwe katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, yakiwemo yale ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na hata dunia kwa umri huo ili baadae iweze kuwa timu yetu ya wakubwa.

Hakuna ubishi kuwa kutokana na vipaji vilivyopo katika timu hiyo, endapo TFF itawekeza zaidi, nasi tutarajia mambo mazuri katika timu yeti ya Kilimanjaro Stars na ile ya Taifa Stars, kwani tutakuwa na wachezaji wenye uwezo na waliolelewa kiprofeshino.

Yote na yote, TFF wanachotakiwa kufanya ni kuendelea kuihudumia timu hiyo na kuhakikisha wanakuwa na kumbumbuku sahihi za wachezaji hao ili kuhakikisha wanawafuatilia kwa karibu.

HATIMAYE safari za ndege kati ya Tanzania na Kenya zimerejea ...

foto
Mwandishi: Tahariri,

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi