loader
Picha

Uzalishaji dawa kwa bangi kuanza rasmi mwakani

SERIKALI ya Uganda inatarajia kuanza uzalishaji na uuzaji wa dawa zitakazotengenezwa kwa kutumia mmea wa bangi mwishoni mwa mwaka ujao.

Hatua hiyo inatokana na taarifa iliyotolewa na wilaya ya Kasese kuwa, ujenzi wa kinu cha kutengenezea dawa hizo umefikia hatua za mwisho kabla ya kuzinduliwa na kuanza kufanya kazi. Kwa mujibu wa taarifa juu ya kinu hicho kinachojengwa katika kata ya Hoima, wilayani Kasese, ujenzi wake unafikia Dola za Marekani milioni 12 sawa na Sh bilioni 44.5 za Uganda.

Mkurugenzi wa kampuni ya Industrial inayomiliki kiwanda cha Hemp ambacho kinashirikiana na kampuni ya Pharma ya Israeli katika mradi huo, Benjamin Cadet, juzi alisema ujenzi wa kiwanda hicho upo katika hatua za mwisho na uzalishaji unatarajiwa kuanza Machi, mwakani kama mambo yatapangwa kama yalivyopangwa.

Kiwanda hicho kimechukua eneo lenye ukubwa wa ekari 12.5 na ndani yake zinapatikana ekari tano zilizosheheni zao la bangi ambalo ndilo litatumika kama malighafi ya kutengeneza dawa hizo. Kiwanda hicho kinatajwa kuwa kikubwa zaidi kuliko vyote barani Afrika na kinatarajiwa kuingiza Sh trilioni moja kwa mwaka.

SERIKALI ya Uganda imesema itatuma Dola za Marekani milioni 60 ...

foto
Mwandishi: KASESE

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi