loader
Picha

Serikali kuongeza uzalishaji mafuta

SERIKALI inatarajia kuongeza uzalishaji wa mafuta kufikia mapipa 200,000 katika miaka miwili ijayo kutoka uzalishaji wa sasa wa mapipa 178,000 kwa siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Mipango,Mafunzo na Utafiti katika Wizara ya Mafuta Sudani Kusini, Arkangelo Okwang Oler akizungumza katika mkutano wa mafuta Afrika Kusini hapa alisema wanajipanga kuongeza uzalishaji wa mafuta.

Alisema katika mipango yao ya muda mrefu wamedhamiria kuzalisha mapipa 350,000 kwa siku. Hata hivyo, hakueleza kufikia muda gani ikiwa ni kiwango ambacho walikuwa wakizalisha mwaka 2012 .

Alisema baadaye mwezi huu watatoa leseni kuendeleza maeneo manane ya uchimbaji mafuta nchini humu katika jitihada za kujenga serikali imara. Nchini humu asilimia 98 ya mapato ya bajeti yanatokana na mafuta lakini kumekuwa na mgogoro wa kiuchumi kwa muda mrefu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe,hivyo kuathiri uchimbaji mafuta.

SERIKALI ya Uganda imesema itatuma Dola za Marekani milioni 60 ...

foto
Mwandishi: CAPE TOWN, Afrika Kusini

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi