loader
Picha

Aliyeongoza Std 7 azitamani Ilboru, Pugu

Mwanafunzi bora kitaifa kwa upande wa wavulana katika mtihani wa darasa la saba 2019 Francis Hussein Gwagi amesema, anataka kuwa mwanafunzi bora mitihani ya sekondari kama ilivyokuwa shule ya msingi.

Mtoto huyo aliyehitimu Shule ya Msingi Paradise mkoani Geita amekuwa mwanafunzi wa pili kitaifa kwa matokeo ya jumla.

Msichana Grace Manga wa Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa kwenye mtihani huo.

Francis amesema, kwa masomo ya sekondari anatamani kusoma katika shule za Ilboru, Mzumbe, Mpwapwa au Pugu kwa kuwa zimekuwa na matokeo mazuri.

Kwa mujibu wa mtoto huyo wakati anasoma shule ya awali alirukishwa darasa na kupelekwa darasa la pili kwa kuwa kila walipofanya mtihani alikuwa anaongoza.

"Na hapo sikuanza vibaya nilimaliza nikiwa number three (namba tatu) darasa la pili, nikaingia darasa la nne nikafanya mtihani wa taifa, straight A in all the subjects (A kwenye masomo yote), mpaka naingia darasa la tano maendeleo yangu yalikuwa mazuri sana, nimeshika number one standard six from January to Desember (kwa kwanza darasa la sita tangu Januari hadi Desemba), na mpaka naingia standard seven I have been number one from January to September (Darasa la saba wa kwanza tangu Januari hadi Septemba"amesema.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

2 Comments

 • avatar
  Danieli eliabi
  15/10/2019

  hongera sana Francs

 • avatar
  Boniphace vedastus
  16/10/2019

  Comment. hongera sana Francis endlea hvyohvyo utafika mbali na mungu hatakupgania zidi kuweka bidii hata kwenye masomo ya sekondary Kwan hata ivyo ni yaleyale inabadlika lugha nakusii soma ok by

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi