loader
Picha

K’njaro, Kigoma na Arusha mkiani kwenye uandikishaji

SIKU moja kabla ya kufungwa kwa uandikishaji wa wapiga kura katika orodha ya wapiga kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wakuu wa mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Kigoma na Arusha wameendelea kusalia katika mtego wa Rais John Magufuli baada ya mikoa yao kushika mkia katika uandikishaji huo.

Akizungumza hivi karibuni Rais Magufuli aliwataka viongozi wa mikoa yote kuwahamamisha wananchi wao kujitokeza na kujiandikisha, huku akiwataka wananchi kutomlaumu kwa hatua zozote atakazozichukua dhidi ya viongozi watakaoshindwa kufikia malengo ya uandikishaji wa wananchi katika mikoa yao.

“Nataka niseme hapa hadharani, ile mikoa ambayo watu wao watashindwa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura nitawashangaa. Ninajua Watanzania hawatanilaumu kwa hatua zitakazochukua,” alisema Rais Magufuli.

Aliyasema hayo Oktoba 12, mwaka huu alipozungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) mkoani Katavi, ambako pamoja na mambo mengine aliwataka viongozi hao kuchangamka na kuwahamasisha wananchi waliopo maeneo yao kujiandikisha.

Tathmini ya siku saba za uandikishaji kuanzia Oktoba 8 hadi 14, iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, imeitaja mikoa ya Kilimanjaro, Kigoma na Arusha kufanya vibaya katika uandikishaji huo huku Kilimanjaro ikishika mkia dhidi ya mikoa yote.

Mbali na mikoa hiyo, halmashauri sita za Mpanda na Mlele mkoani Katavi, Kibiti mkoani Pwani, Ngorongoro mkoani Arusha, Songwe na Mbozi zilizopo mkoani Songwe, zinaongoza kwa kufanya vibaya katika uandikishaji huo zikiwa na wastani wa asilimia chini ya 50. Kwa mujibu wa Jafo, Mkoa wa Kilimanjaro unashika mkia baada ya kufikisha wastani wa asilimia 48 kutokana na wapiga kura 446,954 iliyowandikisha, ikifuatiwa na Kigoma iliyoandikisha wapiga kura 555,856 sawa na asilimia 53 na Arusha iliyowandikisha wapiga kura 551,614 sawa na asilimia 59.

“Kimsingi uandikishaji huu bado ni mdogo kulingana na matarajio katika mikoa hiyo, hivyo nawaomba wakuu wa mikoa hiyo na watendaji wa ngazi zote kuzidi kutoa hamasa kwa wananchi wao wajitokeza na kujiandikisha kabla ya kufungwa kwa zoezi hili Oktoba 17,” alisema Jafo.

Aidha, aliitaja mikoa iliyofanywa vizuri ikioongozwa na Pwani uliofanikiwa kuwaandikisha wapiga kura 4,736,639 sawa na asilimia 80 ya wananchi waliokusudiwa, Dar es Salaam ikishika nafasi ya pili kwa kuandikisha wapiga kura wapatao 2,648,820 sawa na asilimia 77 ya makusudio. Jafo aliitaja mikoa mingine kuwa ni Tanga unaoshika nafasi ya tatu kwa kuandikisha wapiga kura 8,231,094 sawa na asilimia 76 huku Mtwara ukishika nafasi ya nne kwa kuandikisha wapiga kura 5,352,523 sawa na asilimia 75.

Alisema Lindi umeshika nafasi ya tano kwa kuandikisha wananchi 3,536,049 sawa na asilimia 75 kama ilivyo kwa Mtwara huku Iringa ukishika nafasi ya sita kwa kuandikisha wapiga kura 3,181,034 sawa na asilimia 70. Aidha, alisema hadi sasa tathimini hiyo inaonesha kuwa kuwa zaidi ya wananchi 15.5 sawa na asilimia 68 wamejiandikisha ili kufikia malengo yaliyowekwa ya kuwaandikisha wapiga kura milioni 22.916 kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi