loader
Picha

Benki ya dunia kutoa Sh bilioni 1 mradi wa elimu

SERIKALI inatarajia kupata Dola za Marekani milioni 500 (zaidi ya Sh bilioni moja) kwa ajili ya mradi wa elimu utakaowasilishwa Benki ya Dunia mwezi ujao.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayewakilisha nchi za Afrika, Anne Kabagambe jijini Washington DC, Marekani.

Pamoja na kuzungumzia mradi huo, pia miradi ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme la Mto Rufiji na miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ilijadiliwa. Mujibu wa taarifa ya Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Mpango alieleza dhamira ya serikali ya kuinua kiwango cha elimu, kwa kutafuta fedha zaidi na mikopo ya masharti nafuu ambayo itaelekezwa kwenye elimu.

‘’Nimemuomba Kabagambe azidi kusisitiza ili Taifa liweze kupata fedha hizi (Dola za Marekani milioni 500) kwa wakati, na tunaamini kwamba fedha hizo zitaidhinishwa na Benki ya Dunia kama tunavyotarajia,” alisisitiza Dk Mpango.

Alisema pamoja na miradi ya elimu, sekta ya nishati ya umeme pia ni muhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa sababu ukipatikana umeme wa kutosha utasaidia kwa vitendo ajenda ya uchumi wa viwanda kwa kuongeza thamani ya mazao na kuboresha huduma za kijamii nchini.

Aliiomba Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa zisaidie kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali hasa katika sekta ya umeme na miundombinu. Aidha, Dk Mpango alieleza kuwa hivi karibuni Benki ya Dunia iliipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 450 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, awamu ya tatu.

“Hivyo kupitia miradi miwili ya Elimu na TASAF, Tanzania inatarajia kupata dola za Marekani milioni 950,” aliongeza Dk Mpango. Kwa upande wake, Kabagambe alielezea kufurahishwa na utekelezaji wa miradi inayofanyika Tanzania kwani alipata fursa ya kuona miradi mbalimbali ikiwamo SGR na miradi inayotekelezwa na Tasaf, na kuelezea kuwa ni miradi ya mfano na kwa nafasi yake ataendelea kuitangaza ili Tanzania ipate fedha zaidi kutekeleza miradi hiyo.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    leonard sapali
    16/10/2019

    HIZO PESA YA TASAFU WAWEKEZE UJEZI WA ZAHANATI NA MADARASA SHULENI WANAPATA HIZO PESA WANANYWEA TU POMBE NA MATUMIZI YA AJABU KUSAIDIKA KADIRI YA MALENGO YA SERIKALI.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi