loader
Picha

Sare ya Stars yampa ahueni kocha

MWISHONI mwa wiki hii, Timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars itakuwa na kibarua kizito dhidi ya Sudan, katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan.

Katika harakati za kujiandaa na mechi hiyo, Stars juzi ilicheza mechi ya kirafiki na Rwanda mjini Kigali na kutoka suluhu. Matokeo hayo yanaonekana kumridhisha kocha wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije na kusema amepata kipimo sahihi kabla ya kucheza na Sudan mechi ambayo Stars inahitaji ushindi wa kuanzia mabao mawili kusonga mbele baada ya kupoteza mechi ya nyumbani kwa bao 1-0.

Ndayiragije alisema waliingia kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Rwanda wakiwa na malengo mawili kwanza kupata ushindi ili kujiweka mazingira mazuri kwenye viwango Fifa na pili kukiandaa kikosi hicho kwa mchezo dhidi ya Sudan.

“Lengo la kwanza tumeshindwa kufanikiwa kwakuwa tumetoka sare na jambo linalofuatia nadhani kwa kiwango kikubwa tumefanikiwa kwa kupata kipimo sahihi cha kuweza kucheza na Sudan kwenye mchezo wa marudiano ugenini,” alisema.

Alisema kwenye mchezo huo kwa asilimia kubwa aliwatumia wachezaji wanaotoka kwenye ligi ya ndani kwa kuwa ndio haswa watakaocheza dhidi ya Sudan.

Kwa upande wake, Kocha wa Amavubi (Rwanda), Mashami Vincent pamoja na kuwa kwenye uwanja wa nyumbani amekubali matokeo na kwamba wamepata ushindani kutoka kwa Tanzania kwa kuwa kikosi chao kimesheheni wachezaji wenye ubora na wana uzoefu.

Alisema na wao kwa upande wao wameutumia mchezo huo kama kipimo cha kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Chan dhidi ya Ethiopia ambapo Amavubi watakuwa nyumbani kuwakaribisha wapinzani wao hao.

Katika mchezo huo Amavubi wanajukumu kubwa la kulinda ushindi walioupata kwenye mchezo wa kwanza wa bao 1-0 ugenini uliopigwa kwenye Uwanja wa Mekelle, Ethiopia.

“Tumepata ushindani lakini kikubwa kama majirani zetu Tanzania na sisi tulikuwa tunatumia mchezo huu kujiweka sawa kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Ethiopia mechi tukayocheza Oktoba 18 hapa nyumbani,” alisema Vincent.

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi