loader
Picha

Simba kujipima na mabingwa wa Burundi leo

BAADA ya kucheza na Mashujaa juzi, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo watakuwa tena kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma kucheza na mabingwa wa Burundi Aigle Noir katika mchezo wa kirafi ki.

Hiyo ni mechi ya pili kwa Simba kucheza kweny uwanja huo baada ya juzi kucheza na timu ya daraja la kwanza ya Mashujaa na kuifunga bao 1-0. Awali, kabla ya kwenda Kigoma, Simba ilicheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Bandari ya Kenya kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kushinda bao 1-0.

Simba, iliyong’olewa mapema kwenye michuano ya kimataifa, inajifua kujiandaa na mechi za Ligi Kuu ambapo Oktoba 23 itacheza na Azam kwenye uwanja wa Uhuru. Akizungumza juzi kocha wa mabingwa hao, Patrick Aussems alisema malengo ya kucheza michezo mfululizo ya kirafiki katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu imesimama kupisha michuano ya kimataifa ni kutengeneza timu imara na kuwapa nafasi wachezaji wasiopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

“Tunacheza michezo mingi ya kirafiki katika kipindi hiki ni kujaribu kuwapa nafasi wachezaji ambao sio chaguo la kwanza kwenye kikosi cha kwanza kuonesha uwezo lakini pili kuzidi kutengeneza timu imara kujipanga na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Aussems.

Alisema pamoja na kipindi hiki baadhi ya wachezaji wake muhimu kuwajibika kwenye majukumu ya timu zao za taifa lakini anakikosi kipana na kwamba ni wakati wa kuwaweka fiti waliobakia kwenye kikosi hicho ili kuona uwezo wao wa kuwatumia kwenye mechi zijazo.

“Bado tunamalengo ya kutetea ubingwa wa ligi lakini ili tuweze kuendelea kubaki kileleni na kufanikiwa kutimiza malengo lazima tufanye vizuri kwa kupata ushindi na kupata mabao ya kutosha tukianza na mchezo ujao dhidi ya Azam FC,” alisema Aussems.

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi