loader
Picha

Yanga yanoa makali kwa Pan African

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Afrika Yanga wanaendelea kujifua kujiandaa na michezo miwili, wa Ligi Kuu Bara na ule wa kimataifa.

Katika maandalizi ya michezo hiyo, Yanga leo itajipima na timu ya Daraja la Kwanza Pan African kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Yanga inatarajiwa kucheza na Mbao Oktoba 22 katika mechi ya Ligi Kuu kabla ya kuvaana na Pyramid ya Misri katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika siku tano baadaye.

Mechi zote zitachezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mechi dhidi ya Pan ni ya pili kwa wiki hii baada ya juzi kucheza na timu nyingine ya daraja la kwanza ya Friends Rangers na kushinda mabao 4-3.

Kocha Msaidizi, Noel Mwandila alisema michezo hiyo imelenga kuwajenga wachezaji na kuwaandaa kwa michezo ijayo hasa ikizingatiwa kuwa kuna waliorudi kutoka majeruhi.

“Ni michezo ya mazoezi kuwajenga wachezaji na kurekebisha makosa yaliyoonekana katika michezo iliyopita kabla ya kuelekea Mwanza, tunaamini itawasaidia kuwa vizuri kistamina,”alisema.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga waliokuwa majeruhi na wamerejea ni Paulo Godfrey, Papy Tshishimbi, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana na Lamine Moro.

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Aarif Pirmohamed
    17/10/2019

    Hopefully this year Yanga should do better in the mainland Premier League of 2019/20.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi