loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majeshi yawakilishe vyema nchini China

Michuano hiyo mikubwa ni sehemu ya kuendeleza umoja na mshikamano kwa majeshi duniani kwa njia ya michezo.

Ushiriki wa timu za Tanzania msimu huu utaendelea kuleta mwanga katika michezo ya majeshi, lakini sio wanatakiwa washiriki bali kurejesha ubora wao uliopotea kwa miaka mingi.

Miaka ya zamani michezo kama riadha wengi waliovuma walikuwa ni wanajeshi, sasa kwanini ishindikane wakati huu ikiwa kuna vijana wengi wamechukuliwa jeshini kwa sababu za kimichezo. Watanzania watafurahi kuona wanafanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Kufanya kwao vizuri kunaweza kuwashawishi viongozi wao wa majeshi waliopo kuongeza timu wakati ujao na pengine kupeleka soka na michezo mingine iliyobaki kwa kuamini kuna vipaji.

Wasiende tu kushiriki na kushangaa wengine, wafanye ile kazi iliyowapeleka kuleta heshima kwa taifa.

Ikiwa watafanya vizuri wataitangaza nchi kimichezo, wataaminiwa na hata baadhi yao wanaweza kupandishwa vyeo.

Siku hizi jeshi limekuwa na utaratibu kwa wachezaji wake hasa wale wanaofanya vizuri katika michezo hupandishwa vyeo.

Hilo lilionekana katika baadhi ya michezo mingine iliyopita namna ambavyo walinufaika kwa kupandishwa vyeo kutokana jitihada zao za kufanya vizuri.

Watanzania wanataka kuona wachezaji wanarudi na medali na vikombe na hivyo, ni vitu muhimu katika michezo.

Haitapendeza katika michezo yote mitatu wakaenda bure na kurudi kama walivyo pasipokuambulia chochote itakuwa ni aibu.

Waliochaguliwa kuwakilisha ni kwamba wanaaminiwa kuwa wataleta matumaini mapya.

Na kufanya kwao vyema kutachangia na wachezaji wengine waliobaki jeshini kuonesha jitihada ili kupata nafasi ya kuwakilisha katika mashindano yajayo.

Sio kwamba hakuna michezo mingine, tumeshuhudia timu za soka, netiboli, gofu zipo na zinashiriki michuano ya kitaifa na ile ya Afrika na hazijapata nafasi ya kwenda huko ila waliopata ni muhimu kuonesha ni kwanini hawakuchaguliwa kimakosa.

NATAKA niwe mkweli kwa nafsi yangu kuwa, hata kama tungekuwa ...

foto
Mwandishi: NA GRACE MKOJERA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi