loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa- Hutajuta ukiwekeza Pwani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema yeyote atakayewekeza mkoani Pwani hatajuta.

Amesema Pwani ni mahali sahihi pa kuwekeza kwenye sekta zote na amewapongeza wote waliowekeza kwenye mkoa huo.

Ameyasema hayo mjini Kibaha wakati anafungua Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani.

“Wekeza Pwani, hamjajutia mkiwekeza Pwani” amesema na ameupongeza uongozi wa mkoa huo kwa kuwatambua wawekezaji na kuwaalika washiriki kwenye kongamano hilo.

“Na mimi nashawishika kuwa Mkoa wa Pwani ni mahali sahihi pa kuwekeza…nataka niendelee kuwashawishi, wekeza mkoa wa Pwani…kwa hiyo nawakaribisha mkoa wa Pwani kwa uwekezaji”amesema.

Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ikiwemo miundombinu ya barabara kwenda maeneo ya uwekezaji, maji na umeme.

“Kila kinapojengwa kiwanda mkoa pamoja na halmashauri mjiridhishe mmejenga barabara za kudumu, nzuri za kwenda huko” amesema na kuzitaka halmashauri zitumie mapato ya ndani kujenga barabara hizo ili zipate fedha zaidi kwenye uwekezaji huo.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi