loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wawekezaji China waenda Pwani kuona fursa

Ujumbe wa watu watano kutoka jimbo la Hebei nchini China leo unafika Kibaha Pwani kuzungumza na uongozi wa mkoa masuala ya biashara na uwekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema mjini Kibaha kuwa, ujumbe huo unaojumuisha viongozi wa Serikali na wawekezaji wakubwa watatu pia utatembelea mabanda kwenye maonesho ya viwanda mkoa wa Pwani.

“Jimbo la Hebei hili ndio jimbo ambalo viwanda karibu almost 80 to 90 percent (karibu asilimia themanini hadi tisini ya) viwanda vya Beijing vilihamishiwa katika jimbo la Hebei sasa wanakuja wajumbe watano”amesema Ndikilo.

Ameiagiza sekretarieti ya mkoa kuwaeleza wageni hao maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji, na kwamba, ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa mkoa wa Pwani na Taifa.

“Tutawapitisha pia kwenye mabanda ya mabenki kuwathibitishia kabisa kwamba wanaweza wakapata mitaji hapa hapa Tanzania na sio lazima wasubiri kwenye maeneo yao”amesema Ndikilo.

Amesema, ujumbe huo pia utapitishwa kwenye mabanda yanayoonesha maeneo yenye ardhi kwa ajili ya uwekezaji ili wafahamu kuna ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza.

“Kwa hiyo ni ugeni mzito, tumewaalika sisi wenyewe ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia sekretarieti ya mkoa na wenye mabanda mjiandae kesho (leo) tukiwaleta hawa wawekezaji kutoka China basi muwe na maelezo ya kutosha, mjipange vizuri, muwape taarifa za kutosha”amesema.

SERIKALI imetumia Sh Bilioni 15 kwa ajili mikopo ya pembejeo ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi