loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Balozi za Tanzania kutangaza fursa Pwani

Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Pwani utafikishwa kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi ili watu wa huko wazifahamu fursa zilizopo waje kuwekeza.

Mkuu wa mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza sekretarieti ya mkoa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili mwongozo huo ufikishwe kwenye balozi hizo.

Jumamosi iliyopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliuzindua mwongozo huo wakati anafungua kongamano la uwekezaji Mkoa wa Pwani.

“Leo tunaweza tukajivunia kwamba sasa tuna mwongozo wa uwekezaji katika mkoa wetu wa Pwani ambao umetokana na mawazo yetu sisi wenyewe, mawazo ya kila mtaalamu katika mkoa wetu wa Pwani. Leo tunaweza tukasema yeyote yule anayetaka kuja kuwekeza katika mkoa wetu wa Pwani afike kwa sababu tayari tuna mwongozo wa uwekezaji katika sekta zote”amesema Ndikilo mjini Kibaha.

Ndikilo ameagiza mwongozo huo uwekwe kwenye tovuti ya mkoa huo, tovuti ya taifa na kwenye ukurasa wa mkoa kwenye mtandao wa kijamii wa instagram.

“Kupitia teknolojia hii na utaalamu huu mwongozo wetu unaweza ukafika mbali kabisa kwa hiyo tujitahidi sana ili isiwe kwamba ni document (nyaraka) ambayo inaweza ikafichwa, iiishie katika makabrasha katika makabati hapana na mimi nilisema nataka kuona things are happening on the ground, tunataka kuona matokeo chanya kwenye jambo hili” amesema.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi