loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usafiri wa umma Kigali kuboreshwa

MAMLAKA ya Kudhibiti Bei Rwanda (Rura) imetangaza kufanya mageuzi ya kuboresha usafi ri wa umma katika jiji la Kigali kuanzia Mei mwakani.

Mabadiliko hayo yaenda sambamba na kuchagua watoa huduma wapya na kufikia Januari mwakani kampuni mpya zitakuwa zimechaguliwa ili kuanza kutoa huduma za usafiri wa umma katika jiji hilo.

Mageuzi hayo yatafanyika kwa kuhusisha muundo mpya wa usafiri wa umma utakaotekelezwa kuanzia mwaka 2020 mpaka 2025. Mkurugenzi Mkuu wa Rura, Patrick Nyirishema, alisema lengo la kufanya mageuzi hayo ni kupanga vizuri na kuweka ratiba nzuri ya usafiri katika jiji hilo.

“Tutaanza usafiri wa umma awamu ya pili, ikiwa na wazo la kuangalia changamoto zilizokuwapo katika awamu ya kwanza na kufanya maboresho ili kurahisisha huduma hiyo,” alisema.

Rura inapanga kuondoa foleni barabarani kwa kutumia usafiri wa umma kwa kuboresha utendaji kazi na kuratibu njia za kutoa huduma. Abiria wamekuwa wakilalamikia huduma duni zinazotolewa na kampuni zinazotoa huduma hiyo na ukosefu wa taarifa za njia zinazotumika.

Mkuu wa Usafirishaji Rura, Asaba Katabarwa, alisema ni muhimu kuwa na mipango madhubuti katika mfumo wa usafiri kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu. Alisema idadi ya watu katika jiji hilo inatarajiwa kuongezeka kufikia milioni 3.8 kufikia 2050 na ili kuweza kuwahudumia vema ni lazima kuwa na mipango madhubuti ya usafiri wa umma.

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imewatoa hofu wananchi wa jumuiya ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi