loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Tanzania ni salama, China njooni muwekeze’

SERIKALI ya mkoa wa Pwani imeueleza ujumbe kutoka China kuwa Tanzania ni eneo zuri zaidi kwa uwekezaji kwa kuzingatia fursa zilizopo, amani na utulivu wa kisiasa na soko la uhakika hivyo wakiwekeza mitaji yao itakuwa salama na watapata faida.

Mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo amesema mjini Kibaha kuwa, ujumbe huo wakiwemo viongozi wa serikali kutoka Jimbo la Hebei na viongozi wa wafanyabiashara wamefurahishwa na fursa za uwekezaji Pwani na wameahidi kutoa mrejesho baada ya muda mfupi ujao.

Ujumbe huo leo umefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuzungumza na uongozi wa mkoa huo kuhusu fursa zilizopo, taratibu za kuwekeza na namna wanavyoweza kufanya biashara nchini.

“Tumewaambia nchi yetu ipo politically stable (kuna utulivu wa kisiasa), lakini pia ni nchi ambayo tuna amani kabisa kwa maana hiyo basi hata mitaji yao wakiwekeza hapa basi hiyo mitaji inaweza ikalindwa” amesema Ndikilo wakati aanazungumza na waandishi wa habari.

Baada ya ujumbe huo kuzungumza na uongozi wa mkoa, mhandisi Ndikilo aliutembeza kwenye mabanda ya maonesho ya pili ya viwanda mkoa wa Pwani.

Uongozi wa mkoa umewaeleza wageni hao kuwa, Pwani ni eneo sahihi kuwekeza kwa kuwa, pamoja na mambo mengine ipo jirani na Dar es Salaam hivyo wana uhakika wa soko la watu takribani milioni tano na pia wanaweza kuuza bidhaa nje ya nchi.

“Ni rahisi kusafirisha kwa bandari ipo Dar es Salaam pale, lakini kuna uwanja wa ndege upo vizuri kabisa, lakini pia tuna SGR tunajenga lakini pia unaweza ukazalisha na ukapeleka kwenye mikoa ya jirani kwa sababu barabara zote zinapita katika mkoa wetu wa Pwani lakini pia unaweza uka-export (ukauza nje ya nchi) kwenye nchi za jirani kama Afrika Mashariki na kati” amesema Ndikilo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo hadi sasa Pwani kuna uwekezaji wa viwanda vitatu kutoka jimbo la Hebei na ujumbe huo umeahidi kuendelea kuwekeza mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi