loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda kufunga maonesho ya viwanda Pwani

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mizengo Pinda kesho anatarajiwa kufunga maonesho ya pili ya viwanda mkoa Pwani.

Mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo amewaeleza waandishi wa habari mjini Kibaha kuwa, zaidi ya viwanda 330 vimeshiriki maonesho hayo yaliyoanza Alhamisi iliyopita na kufunguliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

“Lengo letu lilikuwa ni kuwa na watu wanaokuja kuyaona zaidi ya laki moja, lakini mbili lakini hiyo yote nafikiri baada ya leo ndio tunaweza tukajua kwamba ni wananchi wangapi wameshiriki katika maonyesho haya” amesema Ndikilo.

Amesema, washiriki wengi wamefurahi kwa kuwa licha ya kuonesha bidhaa lakini pia wamefanya biashara sanjari na kuvitambulisha vitu ambavyo vilikuwa havijulikani.

Kwa mujibu wa Ndikilo, mkoa huo umebaini kuwa, maonesho ya bidhaa zinazozalishwa viwandani ni njia mojawapo ya kukuza biashara za wawekezaji na kutatua changamoto zinazowakabili.

Amesema maonesho ya kwanza ya viwanda ya mkoa huo mwak jana yalileta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuvipatia viwanda masoko wakiwemo wateja kutoka mikoa mbalimbali.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi