loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda ataka viwanda viguse maisha ya watu

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwenye mkoa wa Pwani itakuwa na maana kama vitagusa maisha ya watu.

Ameyasema hayo mjini Kibaha wakati anafunga maonesho ya pili ya viwanda mkoa wa Pwani.

Amebainisha kuwa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano unataka viwanda vitumie rasilimali inayotokana na shughuli za wananchi wakiwemo wakulima, wafugaji na wavuvi.

Amesema miongoni mwa malengo ya mpango huo ni kuufungamanisna uchumi na maendeleo ya watu wakiwemo wajasiriamal ili uwe na maana.

“Kwa hiyo uchumi tunaozungumza kuujenga katika mkoa wetu wa Pwani kupitia viwanda lazima kwa kweli uwe na muunganiko mkubwa na matatizo yanayokabili makundi haya ndipo mtaona maendeleo yale yanakuwa na maana zaidi” amesema.

Kabla ya kuyasema hayo Pinda alitembelea mabanda ya maonesho hayo yaliyoanza Alhamisi iliyopita na kufunguliwa na Makamu wa Rais Samia Suhulu Hassan.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu ‘Ijenge Tanzania, Wekeza Pwani Mahali Sahihi kwa Uwekezaji’ yamehishirikisha wenye viwanda 329 kutoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga, na Morogoro.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi