loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda- Magufuli alifanya uamuzi mgumu

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema, Rais John Magufuli alifanya uamuzi mgumu kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme kwenye Bonde la Mto Rufiji.

Amesema mjini Kibaha kuwa, mradi huo utakaozalisha megawati 2,115 ni miongoni mwa miradi ya kimkakati itakayokuwa na matokeo makubwa kwenye ujenzi wa sekta ya viwanda na nyingine.

Ameitaja miradi mingine kuwa ni kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya, na kujenga reli ya kati ya kisasa.

“Ni miradi ya kimkakati kweli kweli maana sio lele mama hata kidogo” amesema Pinda mjini Kibaha wakati anafunga maonesho ya pili ya viwanda mkoa wa Pwani.

Amesema mradi wa kuzalisha umeme kwenye bwawa la Nyerere unamfurahisha, una hadithi ndefu na kulikuwa na maneno mengi kuhusu gharama na uharibifu wa mazingira.

“Utafikiri la kwao, sasa bwana mkubwa alipoingia pale akawasikiliza akasema ninyi watu wa ajabu sana, kwa nini msihangaike na ya kwenu huko mnafuata ya kwangu. Wataalamu wakamuelimisha vizuri akakuta kumbe hata kule kulalamikia kwamba kunaharibu ni asilimia ndogo sana ya pori lile la Selous, ndogo sana, akasema mimi naendelea, ni mradi wa Watanzania, najua manufaa yake ni nini. Na mradi ule unaenda na amedhamiria utakwisha”amesema Pinda.

Amesema mrai huo ukikamilika viwanda vitakuwa na uhakika wa umeme na amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu aliofanya.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi