loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda ataka taasisi wezeshi eneo moja

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ameuagiza mkoa wa Pwani uanzishe ofisi itakayoziweka pamoja taasisi zote zinazowezesha uwekezaji ili kupunguza usumbufu kwa wawekezaji.

Ametoa agizo hilo kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mjini Kibaha wakati anafunga maonesho ya pili ya viwanda mkoa wa Pwani.

“Huu mfumo niliouaona kwa one stop center nataka ujidhihirishe sasa kwa maana ya ofisi katika mkoa wa Pwani, watu wakija waseme nenda Pwani ukitaka kuona kinachoendelea ni nini, tukifanikiwa hilo utaona kabisa kitu hiki kimekusaidia sana” amesema Pinda.

Ameeleza kufurahishwa na banda lilizoziweka pamoja taasisi hizo wakati maonesho hayo yaliyoanza Alhamisi iliyopita na amebainisha kwamba, hili lisipofanyika mwekezaji anachoka kuzunguka hata kabla ya kuwekeza.

“Na nimewaomba sana, isitoshe tu kuwaoneni hapa kwenye maonyesho haya ndani ya banda moja lakini jambo hili limesisitizwa sana na Serikali zilizopita na Serikali ya Awamu ya Tano kuwa na kitu tunakiita a one stop center mwekezaji anapokuja matatizo yatatuliwe kwenye eneo moja tu kwa kuwakuta wote wahusika katika eneo hilo” amesema Pinda.

Ameutaka Mkoa wa Pwani uwe mfano kwa mikoa mingine kwa kuondoa usumbufu kwa wawekezaji.

"Maana umeshaanza na viwanda, mwekezaj anataka kuja kuwekeza, ukifanya lile utaona wengi watapenda kuja kwenye mkoa wako kwa sababu umejenga mfumo mzuri” amesema Pinda.

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi