loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

MAFURIKO TANGA: Polisi yafuatilia ‘Noah iliyotumbukia mtoni’

JESHI la Polisi mkoani Tanga linafuatilia taarifa zinazoeleza kuwa gari aina ya Noah likiwa na abiria kadhaa limetumbukia mtoni baada ya daraja kukatika wilayani Handeni na kukwamisha shughuli za usafiri.


Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tanga zimeathiri mawasiliano kati ya mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha na nchi jirani, Kenya, baada ya kuharibika miondombinu ya barabara. 


HabariLeo lililazimika kumpigia simu Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Edward Bukombe kwa lengo la kuthibitisha taarifa hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii leo, Jumamosi (Oktoba 26, 2019) na kusema: “nipo njiani kuelekea huko. Kwa sasa sina taarifa kamili,” na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya kufika katika eneo la tukio.


Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kuwa Polisi wamekesha na abiria waliokwama barabarani na hadi sasa usalama umeimarishwa kuhakikisha kuwa hawapati misukosuko wakati wakisubiri hatima ya safari zao.


“Wote wako salama, polisi wamekesha nao na hadi sasa hakuna uhalifu uliotokea,” alisema Kamanda.
HabariLeo itaendelea kufuatilia taarifa zaidi mara Kamanda Bukombe akifika katika eneo hilo.

MGOMBEA urais  wa Zanzibar aliyepitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), ...

foto
Mwandishi: MWANDISHI WETU

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi