loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mvua yazidi kuleta maafa, 10 watumbukia korongoni

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Tanga zimeleta athari mbalimbali mkoani humo ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya watu 10, kukatisha mawasiliano na wananchi kukosa makazi.

Watu hao 10 walipoteza maisha baada ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T890 CCX kutumbukia kwenye korongo lilosababishwa na kukatika daraja kipande cha barabara ya Handeni-Korogwe eneo la Sindeni kutokana na mafuriko ya maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Mbali na kusababisha vifo mvua hiyo pia imesababisha watu kukosa makazi na wengine kukwama wakiwa safarini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kubainisha kuwa kati ya watu hao 10, watu wazima ni nane na watoto wawili.

Eneo hilo la barabara limekatika usiku wa kuamkia jana na ajali imetokea alfajiri ya jana. Idadi hiyo ya vifo inafikisha idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua hizo tangu zilipoanza kunyesha kufikia 21, wilayani Korogwe wamekufa watu 11 kati yao sita kwa kuangukiwa na nyumba na watoto watano kusombwa na mafuriko.

Aidha mbali na vifo hivyo pia mamia ya wakazi katika wilaya za Korogwe, Kilindi, Muheza na Handeni wamekosa makazi kutokana na makazi yao kuzingirwa na maji.

Changamoto nyingine ni kukatika kwa mawasiliano ya barabara katika barabara kuu za Tanga- Segera eneo la daraja la Hale katika mto Pangani, barabara ya Segera Korogwe katika daraja la Mandera, eneo jingine ni daraja la Kilole katika mzunguko wa barabara ya kati ya Kilole ,njia panda ya Handeni na Manundu.

Maeneo mengine barabara ya Korogwe- Handeni eneo la Komsala na Misima ambapo eneo la barabara limekatika, barabara ya Handeni Kilindi katika daraja la Mabalanga ambapo daraja na madaraja mengine yamejaa maji na barabara ya Handeni - Turiani eneo la Kideleko ambapo daraja limekatika.

Eneo jingine ni barabara ya Muheza Amani nako mawasiliano ya barabara yamekatika kutokana na barabara kuwa na hali mbaya na magari yanapata changamoto ya kupita.

Kutokana na hali hiyo wasafiri katika mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania (Tanga, Aru sha na Kilimanjaro) na Dar es salam kupitia barabara kuu za Korogwe-Handeni-Mkata na Korogwe-Segera- Tanga wamekwama.

Inasemekana dereva wa gari hiyo inayofanya safari zake kati ya Handeni na Korogwe alijikuta akitumbukia kwani hakujua eneo hilo kama limekatika Athari zilizopo ni kujaa kwa maji katika makazi ya watu na kukatika kwa mawasiliano kati ya wilaya moja na nyingine na kukatika kwa umeme.

Wilaya ambazo zimeendelea kuathirika na mafuriko hayo ni wilaya za Handeni, Korogwe, Kilindi na Muheza na mawasiliano ya barabara zinazounganisha sehemu mbalimbali katika wilaya hizo kukatika.

WATOTO 84,625 waliokuwa na utapiamlo mkali, wametibiwa kuanzia mwanzoni mwa ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Tanga

1 Comments

  • avatar
    Jitulamungu odungo
    29/10/2019

    CommentOktoba 2019 Vyanzo vya habari vinaripoti mafuriko katika maeneo mengi nchini Tanzania kutokana na mvua kubwa. Mvua inaripotiwa kuendelea kama usumbufu unaoendelea unaohusiana na mafuriko. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko ni pamoja na wilaya za Handeni na Korogwe katika Mkoa wa Tanga. Vyanzo vya habari vinaripoti kwamba watu 14 wameuawa katika matukio yanayohusiana na mafuriko katika Wilaya ya Handeni. Vifo vikuu vilitokea katika kitongoji cha Kaunti ya Sindeni, na miili miwili iligunduliwa kwenye uwanja wa Wandama St katika Kata ya Kwenjugo. Watu kumi waliuawa huko Sindeni baada ya kusafirishwa na abiria waliohusika katika ajali na kutumbuliwa kwenye maji ya mafuriko. Katika Wilaya ya Korogwe, makazi mengi yalifurika na wakaazi wakakimbia makazi yao. Watu wanaosafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro, na kaunti zingine za jirani kwenda Dar es salaam wameshikiliwa katika Wilaya ya Korogwe. Uharibifu wa madaraja, barabara, na mashamba ya mazao yameripotiwa katika mkoa wote. Kwa jumla, watu 44 waliuawa nchini Tanzania katika matukio yanayohusiana na mafuriko. Umma unashauriwa kuangalia ripoti za hali ya hewa kwa eneo hilo na Epuka kuendesha gari kupitia barabara zilizo na mafuriko. Ilisasishwa 29 Oktoba 2019 saa 11:09. Maelezo yenyewe NC4, unaenda kwenye wa kuripoti juu juuuniuni. mfuko Wa waziri mkuu kwaajili ya maafa uwasaidie mana ndio kaziyake hata bajeti bungeni hupangwa. maoni yangu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi