loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ulawiti watoto watikisa Mombasa

VITENDO dhalimu vya kulawiti watoto vilivyokuwa vikiitesa Mombasa katika miaka ya nyuma, sasa vimerejea kwa kishindo, ambapo inaelezwa kwa kiwango kikubwa vinatekelezwa na watu wazima na watoto kwa watoto.

Kwa mujibu wa utafiti ulioendeshwa na taasisi isiyo ya serikali ya haki za uzazi ya ICRH katika miji ya Pwani nchini Kenya, kwa kiasi kikubwa vitendo hivyo vinafanywa na majirani, watu wa familia moja na ndugu wa upande wa wazazi wa kiume.

Miongoni mwa watu waliohojiwa katika utafiti huo ni wauguzi wa vituo vya kuwapokea waathiriwa wa ubakaji katika miji ya Pwani ya Kenya. Muuguzi Mshauri katika kituo cha kuwahudumia waathiriwa wa ubakaji na dhuluma nyingine za kingono katika hospitali kuu ya ukanda wa Pwani ya Makadara, Saida Mwinyi, alisema watoto wanaolawitiwa ni wa kike na kiume.

Aliwaambia maofisa wa utafiti huo kuwa, matukio hayo ni mengi katika majimbo ya Kisauni na Nyali katika mji wa Mombasa. “Kwa bahati mbaya jamii imekuwa na siri kubwa katika kuwafichua wanaojishughulisha na vitendo hivi vya kikatili,” alisema Mwinyi.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: MOMBASA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi