loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Deni la ada uanachama EAC laitoa jasho Burundi

BURUNDI imedhamiria kulipa madeni inayodaiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kulipa Dola za Marekani milioni 1.7 wiki iliyopita.

Mpaka Juni, mwaka huu, nchi hiyo ilikuwa imelipa Dola 408,548, ikiwa ni ada ya uanachama, sawa na asilimia tano ya ada wanayotakiwa kulipa. Waziri wa EAC wa Burundi, Isabelle Ndahayo (pichani), amesema bado wanatakiwa kulipa asilimia mbili ya malimbikizo ili kuanza kulipa mchango wa mwaka huu wa fedha.

“Serikali imejizatiti kulipa malimbikizo yote tunayodaiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani tunatakiwa kulipa asilimia mbili tu ya malimbikizo ili tuanze kulipa michango ya mwaka huu,’ alisema.

Waziri huyo alisema hayo wakati akiwasilisha ripoti ya shughuli za serikali zilizofanyika katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha. Alisema serikali imelipa dola za Marekani milioni 1.7 za malimbikizo yake wiki iliyopita, jambo linaloonesha jinsi nchi hiyo ilivyo na nia ya dhati kulipa malimbikizo yote.

Oktoba mwaka jana, Ndahayo alieleza kuwa, nchi hiyo itakuwa imelipa malimbikizo yote ya EAC ifikapo Desemba, mwaka huu. Barua iliyowasilishwa kwa waziri huyo Januari 17 mwaka huu na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Kirunda Kivijinja, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, iliitaka Burundi kulipa malimbikizo yake ya dola za Marekani milioni 25 ili kuiwezesha jumuiya kutekeleza majukumu yake.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi