loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Umeme wa Uganda sasa kusambazwa Sudan Kusini

WAZIRI wa Umeme na Mabwawa, Dhieu Mathok Diing, ametangaza kuzinduliwa kwa usambazaji umeme kutoka nchi jirani ya Uganda mpaka miji ya mpakani ya Nimule, Kaya na Kajo-Keji.

Diing alisema uzinduzi huo umefanyika Nimule, ikiwa ni makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Alisema makubaliano hayo yanaitaka Uganda kusambaza nishati hiyo katika miji mitatu ya Nimule, Kaya na Kajo-Keji.

“Tumesaini makubaliano ya pamoja ya kuuziwa nishati hiyo na sasa ujenzi wa vituo umeanza na serikali ya Uganda imekubali kujenga njia za umeme,” alisema.

Alisema awamu ya kwanza itakuwa Nimule, ya pili Kaya na ya tatu Kajokeji na Uganda itagharamia gharama zote.

“Uganda itatekeleza mradi huu, hatutalipa kama Sudan Kusini bali tutarudisha gharama kutokana na kukusanya malipo ya umeme,” alisema.

Mwaka 2017, nchi hizo mbili zilisaini makubaliano ya maendeleo ya miundombinu na usambazaji umeme mipakani, ikiwa ni ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa hayo.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: JUBA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi